• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema hatua nzuri za kuhakikisha haki za binadamu zaweza kupunguza athari za COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-09-15 17:15:23

    Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu Bibi Michelle Bachelet amesema, hatua nzuri za kuhakikisha haki za binadamu zinaweza kupunguza athari za COVID-19. Amesema mfumo mzuri wa baadhi ya nchi wa huduma ya matibabu na utoaji wa huduma kwa jamii umelinda vizuri zaidi haki za msingi za binadamu katika kipindi cha janga la virusi hivyo.

    Bibi Bachelet pia amesema, athari za janga hilo zinatofautiana kati ya makabila tofauti, na watu wenye hadhi tofauti za kijamii na kiuchumi, hivyo, nchi husika zinapaswa kuchukua hatua halisi kujenga jamii yenye usawa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako