• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya maambukizi ya COVID-19 nchini India yazidi milioni 5

    (GMT+08:00) 2020-09-17 09:52:02

    Idadi ya watu waliothibitishwa kuambukiza COVID-19 nchini India imeongezeka na kuwa zaidi ya milioni 5, na India imekuwa nchi ya pili yenye wagonjwa zaidi ya milioni 5 baada ya Marekani.

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya afya ya India zimeonesha kuwa, idadi ya jumla ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona imefikia 5,020,359, na idadi ya vifo vya watu kutokana na virusi hivyo imefikia 82,066.

    Tangu hivi karibuni India ilipoanza kulegeza hatua za karantini, idadi ya maambukizi mapya ya COVID-19 kwenye baadhi ya miji mikubwa imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Hatua ya mji wa New Delhi kurudisha shughuli za kiuchumi na kijamii, na kuzinduliwa tena kwa huduma ya subway kumesababisha ongezeko la kasi la maambukizi mjini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako