• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafungwa wengine watano waliotoroka jela nchini Uganda wauawa, mmoja akamatwa

    (GMT+08:00) 2020-09-21 09:23:36

    Wafungwa wengine watano waliotoroka jela nchini Uganda wameuawa, na kufanya idadi ya wafungwa waliouawa kufikia 13 katika msako unaoendelea wa kuwakamata wafungwa 219 waliotoroka jela wilayani Moroto.

    Msemaji wa Jeshi la Uganda Flavia Byekwaso ameliambia Shirika la Habari la China kwa njia ya simu kuwa, vikosi vya jeshi la ulinzi la Uganda vimewaua wafungwa watatu katika msako wa wafungwa waliotoroka jela ya Singila Jumatano mchana.

    Amesema jumla ya wafungwa kumi wamekamatwa tena mpaka sasa, na kuongeza kuwa jamii ya eneo hilo inasaidiana na jeshi kuwasaka watoroka hao, ambao wengi wao ni wapiganaji wa kabila la Karimojong na wezi wa ng'ombe waliofungwa kutokana na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako