• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TikTok yatarajia kufikia makubaliano ya pande tatu ili kuondoa wasiwasi wa usalama uliotolewa na Marekani

    (GMT+08:00) 2020-09-21 09:24:04

    Kampuni ya mtandao wa kijamii wa TikTok imeeleza matumaini yake kuwa makubaliano yaliyofikiwa na kampuni mama ya China ByteDance pamoja na Oracle na Walmart yatasaidia kuondoa wasiwasi wa kiusalama wa uongozi wa Marekani, na kujibu swali kuhusu hatma ya TikTok nchini Marekani.

    Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa Jumamosi na makao makuu ya kampuni hiyo jijini Los Angeles Marekani, ikiwa ni saa chache baada ya rais Donald Trump kusema ameridhia makubaliano kati ya pande hizo tatu.

    Ikiwa sehemu ya makubaliano hayo, Oracle itasimamia data za watumiaji wote wa TikTok nchini Marekani, na kuangalia usalama wa mifumo ya computer ili kuhakikisha mahitaji ya usalama wa taifa la Marekani yanatimizwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako