• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kuheshimu uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-09-21 10:31:29

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun amesema, China inapenda kuheshimu uamuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutochukua hatua yoyote kutokana na madai ya Marekani dhidi ya Iran.

    Hivi karibuni, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo alisema, kutokana na utaratibu wa kuanzisha tena kwa haraka vikwazo dhidi ya Iran uliowekwa katika azimio namba 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran vilivyotekelezwa kabla ya kufikiwa kwa makublaiano ya nyuklia ya Iran mwaka 2015 vimeanza tena rasmi jana, na Marekani itaweka vikwazo mfululizo dhidi ya Iran katika siku za karibuni.

    Balozi Zhang Jun amesema, mwezi Mei mwaka 2018, Marekani ilijitoa kwenye makubaliano ya suala la nyuklia la Iran, hivyo madai yake ya kurejesha utaratibu huo haliendani na sheria.

    Balozi Zhang amesisitiza kuwa, kutokana na sababu hizo, utaratibu huo haujaanza kutekeleza, na Baraza la Usalama litaendelea kusimamisha vikwazo dhidi ya Iran kwa mujibu wa azimio la 2231.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako