• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Klabu ya Simba inatarajiwa kufanya sherehe mjini Morogoro

    (GMT+08:00) 2020-10-02 19:15:50

    TIMU ya Simba inatarajia kufanya sherehe ya ubingwa na mashabiki wake leo mkoani Morogoro, kabla ya kuelekea jijini Dodoma kuifuata JKT Tanzania. Timu hiyo iliyotarajiwa kuondoka leo asubuhi itakuwa Morogoro baada ya sherehe hizo wakiwa na kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, na kesho alfajiri wataanza safari ya Dodoma. Sherehe hiyo ni mwendelezo wa kutoa nafasi kwa mashabiki wao kupiga picha na kombe la ubingwa kama walivyofanya katika sehemu nyingine.

    Simba ambayo imetoka kupata ushindi mnono katika mechi zake mbili zilizopita nyumbani, itacheza na JKT Tanzania Jumapili hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Mkuu wa Idara ya Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, alisema wameamua kupitia Morogoro kutokana na ombi la mashabiki wao, wanaotaka kufanya sherehe ya ubingwa. Manara amesema wanakwenda kucheza mechi ya mwisho kabla ya kukutana na watani wao Yanga tarehe 18, kwa sababu mchezo wa tarehe 11 umeahirishwa kutokana na ratiba ya mchezo wa timu ya Taifa, Taifa Stars.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako