• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asisitiza kukumbuka ushindi mkubwa na kusonga mbele kwa hatua madhubuti

    (GMT+08:00) 2020-10-23 18:03:34

    Mkutano wa kuadhimisha miaka 70 ya Jeshi la China kusaidia Korea Kaskazini kupambana na uvamizi wa Marekani umefanyika leo Oktoba 23 hapa Beijing. Rais Xi Jinping ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amehudhuria na kuhutubia mkutano huo. Rais Xi amewasisitiza wachina kukumbuka mioyoni ushindi mkubwa wa jeshi la China kwenye mapambano dhidi ya uvamizi wa Marekani nchini Korea Kaskazini, wawe na ushupavu na busara kwenye mapambano na kuendelea kusukuma mbele kwa hatua madhubuti jukumu kuu la kuendeleza ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya.

    Leo asubuhi mkutano wa kuadhimisha miaka 70 ya Jeshi la China kuisaidia Korea Kaskazini kupambana uvamizi wa Marekani umefanyika kwenye Jumba la Mikutano la Watu wa China hapa Beijing. Viongozi wa chama na serikali, maveterani wa jeshi la China walioshiriki kwenye vita hiyo, wawakilishi wa jamaa za wanajeshi wa China waliopoteza maisha katika vita hiyo na wajumbe kutoka sekta mbalimbali za Beijing walikaa kimya ili kutoa heshima kwa mashujaa wa China waliopoteza maisha kwenye vita hiyo.

    Akihutubia mkutano huo, Rais Xi Jinping amewakumbuka wanamapinduzi wakongwe, makamanda na askari wa jeshi la China na mashujaa waliojitoa muhanga kwenye mapambano dhidi ya uvamizi wa Marekani nchini Korea Kaskazini.

    "katika miaka 70 iliyopita, kamwe hatuwezi kuwasahau mashujaa wetu waliojitoa muhanga katika vita ya kuisaidia Korea Kaskazini kupambana na uvamizi wa Marekani. Mashujaa zaidi ya laki moja na elfu 97 walipoteza maisha yao kwa ajili ya taifa, wananchi na amani. Michango mikubwa ya mashujaa hao itakumbukwa kizazi baada ya kizazi, na moyo wa ushujaa unaenziwa daima!"

    Rais Xi amesema ushindi mkubwa wa jeshi la China kwenye mapambano hayo ni ilani ya watu wa China kuinuka mashariki mwa ulimwengu baada ya kupata uhuru, na pia ni mnara muhimu wa taifa la China kuelekea ustawi mpya.

    "Baada ya vita hii, watu wa China walivunja njama ya wavamizi ya kuweka vikosi mpakani mwa China na halafu kuimaliza China mpya baada ya kuasisiwa kwake, mabeberu hawajathubutu kujaribu tena kuivamia China mpya kwa nguvu, na tangu wakati huu ndipo China mpya ikainuka kwa uimara. Ushindi wetu katika vita hiyo, ulilinda ardhi na mamlaka ya taifa na kutuletea amani na usalama, na umeonesha kikamilifu nia thabiti ya watu wa China ya kutosalimu amri mbele ya nguvu ya ukatili."

    Rais Xi amebainisha kuwa katika miongo kadhaa iliyopita tangu vita hiyo kutokea, ujamaa kwenye umaalumu wa China umeingia kwenye zama mpya, na taifa la China limepiga hatua kubwa kutoka kuinuka, kutajirika hadi kuwa na nguvu. Amesema China inapaswa kukumbuka magumu iliyopitia na ushindi iliopata kwenye mapambano hayo, na kuendelea kuendeleza ujumaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya.

    Pia amesisitiza kuwa amani, maendeleo na ushirikiano ni mwelekeo sahihi wa dunia ya sasa, na vitendo vyovyote vya upande mmoja, kujilinda kibiashara, kushinkiza au kufanya umwamba na ubabe dhidi ya nchi nyingine, vyote ni njia zisizopitika.

    "China siku zote inatekeleza sera ya ulinzi ya kujilinda, na jeshi la China siku zote ni nguvu thabiti ya kulinda amani ya dunia. China kamwe haitafuti umwamba wala kupanua ardhi, na inapinga kithabiti sera za umwamba na siasa ya ubabe. Kamwe hatutaruhusu mamlaka ya nchi, usalama wa taifa na maslahi ya maendeleo viharibiwe, na wala hatutaruhusu mtu yeyote au nguvu yoyote kuvamia na kufarakanisha ardhi ya nchi yetu. Endapo hali mbaya kama hizi itatokea, watu wa China hakika watajibu kithabiti na kwa hatua kali!"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako