• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kipa Marc- Andre ter Stegen arejea tena kikosini Barcelona

    (GMT+08:00) 2020-11-03 17:07:09

    Kipa namba moja wa Klabu ya Barcelona Marc- Andre ter Stegen, ameanza mazoezi na kikosi hicho baada ya kuwa nje kwa muda mrefu. Ter Stegen alitupwa nje baada ya kuumia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita baada ya kipigo cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich. Kipa huyo ameanza mazoezi ndani ya kikosi cha timu hiyo, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita baada ya kuwa nje kwa muda mrefu. Kwa sasa Barcelona wanamtumia Neto kama kipa namba moja ndani ya kikosi hicho badala ya Ter Stegen. Hata hivyo, Barcelona pia ilithibitisha kuwa beki wake Samuel Umtiti pia amepona na sasa yupo kikosini akifanya mazoezi na kikosi hicho kwa sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako