• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Timu ya Wasichana chini ya Miaka 17 ya Tanzania yaishushia kichapo cha mbwa Comoros

    (GMT+08:00) 2020-11-05 16:56:12

    Kikosi cha Timu ya Wasichana chini ya Miaka 17 cha Tanzania jana kiliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Comoros kwenye michuano ya COSAFA. Warembo hao wakiwa ni waalikwa kwenye michuano hiyo inayofanyika Afrika Kusini, wameishushia kichapo hicho Comoros kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Oval. Mabao ya Tanzania yalifungwa na Aisha Masaka aliyetupia mawili dakika ya 20 na 59 huku Joyce Fred dakika ya 71, Mwanamvua Seif dakika ya 82 na Protasia Mbunda walitupia bao mojamoja. Lile la Comoros lilifungwa dakika ya 26 kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Nassrat Mistoishhi lilidumu mpaka dakika ya 90 na kuwafanya wakubali kichapo kutoka kwa Tanzania. Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Edna Lema amesema kuwa maandalizi mazuri yamewapa matokeo chanya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako