• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Dulla Mbabe aondolewa kuzipiga na bondia Kabangu kutoka DRC nafasi yake yazibwa na Hussein Itaba

    (GMT+08:00) 2020-11-05 16:56:33

    Bondia maarufu Bongo, Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe' ameondolewa kuzipiga na bondia kutoka DR Congo Alex Kabangu na nafasi yake imechukuliwa na Hussein Itaba. Pambano hilo limepangwa kufanyika Novemba 13 ukumbi wa Next Door Arena, Oysterbay na siku hiyo pia bondia nyota nchini Tanzania Hassan Mwakinyo atazipiga na bondia Jose Carlos Paz kutoka Argentina akiwania mikanda miwili. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Jackson Sport, Kelvin Twissa amesema kuwa mabadiliko hayo ni kawaida kutokea katika masuala ya ngumi za kulipwa na wao wamefanya hivyo kwa lengo la kupanua wigo na kujenga heshima katika ngumi za kulipwa nchini Tanzania, na sasa bondia huyo (Itaba) ameanza mazoezi kwa ajili ya kupambana na Kabangu. Hivi karibuni, Mbabe alipigwa kwa pointi dhidi ya bondia Bek Nurmaganbet mjini Atyrau, Kazakhstan. Amesema kuwa maandalizi ya mapambano ya 'Dar Fight Night' yanaendelea vizuri huku bondia bingwa wa mabara wa uzito wa superwelter Hassan Mwakinyo akijifua vikali. Mbali ya kutetea mkanda huo, Mwakinyo pia atawania ubingwa wa mabara wa uzito huo huo wa Chama cha IBA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako