• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Amos Kipruto aahidi makubwa kwenye mbio za Marathon za Valencia

    (GMT+08:00) 2020-11-05 16:56:55

    Mshindi wa nishani ya shaba katika marathon ya dunia mwaka 2019, Amos Kipruto amesema analenga kuimarisha matokeo yake kwa kusajili muda bora zaidi kwenye makala yajayo ya mbio za Marathon za Valencia. Kipruto atapania kutumia mbio hizo za Valencia Disemba 6 nchini Uhispania kuimarisha muda wake bora wa saa 2:05.43 aliosajili kwenye Marathon ya Amsterdam 2018. Mwanaridha huyo amekuwa akishiriki mazoezi ya kina katika eneo la Kapsabet, Kaunti ya Nandi kwa miezi kadhaa saa tangu alipoambulia nafasi ya 18 kwenye mbio za Marathon ya Tokyo Machi 2020 baada ya kusajili muda wa saa 2:08:00. Japo itakuwa mara yake ya kwanza kushiriki Valencia Marathon, atapania kujinyanyua baada ya kuambulia nafasi ya 18 kwenye mbio za Marathon ya Tokyo mnamo Machi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako