• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kibrua cha Ole Gunnar Solskjaer chanukia kuota mbawa

    (GMT+08:00) 2020-11-06 17:02:47

    Manchester United wamemuendea Mauricio Pochettino ili kuchukua nafasi ya kocha aliyopo sasa Ole Gunnar Solskjaer. Solskjaer yupo kwenye presha kubwa ya kibarua chake kuota nyasi kufuatia matokeo mabaya ya 'back-to-back' dhidi ya Arsenal kwenye Premier League na yale ya Istanbul Basaksehir katika Champions League hivyo kujikuta akiingia kwenye kitabu cha wanaotarajiwa kutimuliwa. Kwa mujibu wa Manchester Evening News, United wamewasiliana na Pochettino kuchukua mikoba, hata hivyo inadaiwa hapo awali Pochettino amewahi kutamani kuifundisha United hivyo wanaamini kocha huyo bado hajabadili maamuzi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako