• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: kikosi cha raga cha Kenya SFX10 chaanza na matumaini makubwa

    (GMT+08:00) 2020-11-06 17:04:11

    SFX10 walianza kampeni zao wiki moja baada ya kuanza kampeni hizo baada ya mwanaraga mmoja wa kikosi chao kupatikana na virusi vya corona. Hata hivyo, walitawala mechi zao zote tatu Novemba 2, 2020 kwa kuwapiga Rhinos 24-5, Phoenix 30-0 na Miami Sun42-5. Kikosi cha SFX10 kinajivunia pia maarifa ya mchezaji Cecil Afrika wa timu ya taifa ya Afrika Kusini almaarufu Springbok Sevens na mwanaraga matata Luke Treharne wa Wales. Mbali na Injera, wanaraga wengine wa Kenya ambao wananogesha kivumbi cha World Tens wakivalia jezi za SFX10 ni Monate Akuei, Willy Ambaka, Oscar Ouma, Oscar Dennis na nahodha wa Shujaa, Andrew Amonde. Kikosi cha SFX 10 kutoka Cape Town, Afrika Kusini kinanolewa na mwanaraga wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Frankie Horne. Amonde ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Shujaa amesema mechi za World Tens nchini Bermuda zinatarajiwa kuwapa jukwaa mwafaka zaidi la kujiandaa kwa michezo ijayo ya Olimpiki jijini Tokyo, Japan mnamo Julai 2021 hasa baada ya kusitishwa kwa duru nne za Raga ya Dunia mwishoni mwa msimu uliopita wa 2019-20.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako