• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu ya Taifa ya Tanzania iko nchini Uturuki ikijiandaa kwa mechi dhidi ya Tunisia

    (GMT+08:00) 2020-11-09 18:32:58

    Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jana Jumapili iliondoka Dar es salaam kwenda Istanbul Uturuki, kuweka kambi ya kujiandaa na mechi na Tunisia ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON). Stars itacheza na Tunisia Novemba 13 ugenini, wakati mechi ya marudiano itachezwa katika Tanzania Uwanja wa Benjamin Mkapa, siku nne baadaye Novemba 17. Kikosi hicho kinachoongozwa na kocha Etienne Ndayiragije, kimeondoka kikiwa na wachezaji wa Simba na Yanga ambao walikuwa na mchezo wa watani wa jadi, uliopigwa jana Jumamosi Novemba 7. Kuelekea mchezo huo, wadau wa soka wamezungumzia mechi ya Stars na Tunisia kwamba itakuwa na ushindani, huku wakitajwa wachezaji wa Simba na Yanga kwamba watakuwa na msaada mkubwa. Hata hivyo uzoefu umeonyesha kuwa mara nyingi kucheza kwenye viwanja vya nchi za kiarabu mechi zinakuwa kali na ngumu kwa timu, huu utakuwa ni mtihani mkubwa kwa kocha Ndayiragije kubadilisha hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako