• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Kiongozi wa kikundi cha madaktari wa China nchini Namibia Chu Hailin 2020-01-24

  Leo ni mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa kichina. Wachina wana desturi ya kukaa pamoja na familia zao ili kusherehekea sikukuu hiyo. Lakini kwa madaktari Wachina wanaotoa msaada wa matibabu barani Afrika, leo ni siku ya kawaida ya kazi.

  • Tanzania yajiunga na China kusherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya 2020-01-20

  Watanzania wamejiunga na marafiki zao wa China kusherehekea sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina inayokaribia kwenye tamasha kubwa la Heri ya Mwaka Mpya wa Kichina 2020. Shughuli hizo zimefanyika nchini Tanzania kwa miaka kumi mfululizo, ambazo zinaonesha kukaribia kwa mwaka mpya wa jadi wa kichina.

  • Mwakilishi maalumu wa China ahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais wa Msumbiji 2020-01-17
  Mwakilishi maalumu wa rais wa China ambaye pia ni naibu spika wa kamati ya kudumu ya bunge la umma la China, Bw. Cai Dafeng, Jumatano alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Filipe Nyusi wa Msumbiji huko Maputo, na kukutana rais Nyusi Alhamisi.
  • China yashiriki katika mageuzi ya kiuchumi ya nchini Djibouti 2020-01-10

  Wakati Djibouti inatumia kwa kikamilifu fursa kubwa ya kiuchumi inayotokana na eneo lake la kimkakati la kijiografia, ushiriki wa China umesaidia matarajio ya nchi hiyo kuwa nchi muhimu kiuchumi, katika biashara na pia mambo ya bahari, ikiunganisha bara la Afrika na Bahari Nyekundu. China imesaidia mageuzi ya Djibouti kupitia ushiriki wake katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli yenye urefu wa kilomita 752 inayoanzia bandari ya Djibouti hadi mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

  • Viongozi wa Djibouti wakutana na waziri wa mambo ya nje wa China 2020-01-10

  Rais Ismail Omar Guelleh wa Djibouti na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Mahamoud Ali Youssouf kwa nyakati tofauti wamekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Djibouti.

  • China na Afrika zaingia kwenye mwongo mpya wa uhusiano wenye nguvu kupitia ushirikiano wenye manufaa 2020-01-07

  Mjumbe wa Taifa wa China ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Bw. Wang Yi leo anaanza ziara ya siku 7 barani Afrika, ikiwa ni ziara yake ya kwanza kwa nchi za nje kwa mwaka 2020. Ziara hii inaashiria miaka 30 mfululizo ambapo waziri wa mambo ya nje wa China ametembelea nchi za Afrika mwanzoni mwa kila mwaka kuanzia mwaka 1991.

  • Chuo kikuu cha Maasai Mara na chuo cha Sayansi cha China chatarajia kujenga kiwanda cha kisasa 2020-01-01
  Chuo kikuu cha Maasai Mara kwa ushirikiano na chuo cha Sayansi cha China kinatarajia kujenga kiwanda cha kisasa cha kutengeneza dawa asili kutoka kwa miti maalum. Kwa sasa, zaidi ya miti 210 ya aina mbali mbali yenye manufaa ya kiafya, imepandwa kwenye bustani maalum katika Chuo hicho.
  • Uchaguzi mkuu wa Guinea Bissau wafanyika bila tukio lolote 2019-12-30
  Vituo vyote vya upigaji kura vimefungwa saa 11 mchana kwa saa za huko nchini Guinea Bissau. Msemaji wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo bibi Felisberta Moura Vaz ameyasema hayo na kukanusha habari kuhusu kuwepo kwa udanganifu katika uchaguzi.
  • Mjumbe wa taifa wa China Bw. Wang Yong akutana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya 2019-12-18
  • Mjumbe wa taifa wa China afanya mazungumzo na waziri mkuu wa Lesotho 2019-12-15

  Mjumbe wa taifa wa China aliyeko ziarani nchini Lesotho Bw. Wang Yong jana alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa Lesotho Bw. Thomas Motsoahae Thabane mjini Maseru.

  • Ubalozi wa China nchini Kenya watoa zawadi za mwaka mpya kwa watoto wa shule ya mtaa wa Mathare
   2019-12-12

  Ubalozi wa China nchini Kenya umetoa zawadi za mwaka mpya kwa watoto wa shule ya Mcedo-Beijing iliyoko kwenye mtaa wa Mathare. Zawadi hizo ikiwa ni pamoja na chakula na vifaa vya michezo zimewafurahisha sana watoto hao.

  • Rais wa Zimbabwe akagua mradi wa jengo la bunge linalojengwa na kampuni ya China 2019-11-28

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amekagua mradi wa ujenzi wa jengo jipya la bunge la nchi hiyo linalojengwa na kampuni ya China na kusifu kasi ya ujenzi huo na manufaa yatakayoletwa kwa watu wa Zimbabwe.

  • Rais wa Zimbabwe akagua ujenzi wa jengo jipya la bunge 2019-11-28

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametembelea eneo la ujenzi wa jengo jipya la bunge linalojengwa kwa msaada wa China, na kuishukuru China kwa msaada inaotoa kwa Zimbabwe katika muda mrefu uliopita.

  • Kampuni ya China kuchimba udongo wa Diatomite nchini Kenya
   2019-11-26

  Kampuni ya Kimataifa ya Madini ya Chuanshan ya China na serikali ya Kenya zimesaini makualibano ya kuchimba udongo wa Diatomite katika jimbo la Baringo lililoko kaskazini magharibi mwa Kenya. Maofisa wa Kenya wamesema mradi huu utahimiza maendeleo ya sekta ya viwanda na uchumi wa jimbo hilo.

  • Ethiopia yatarajia kuwa kitovu cha biashata ya mtandaoni Afrika 2019-11-26
  Ethiopia inatarajia kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mtandaoni barani Afrika baada ya kusaini makubaliano ya kuanzisha kituo cha biashara ya mtandao ya Kimataifa eWTP na kampuni ya Alibaba ya China.
  • Askari 240 wa ulinzi wa amani wa China wamaliza kazi yao nchini Sudan Kusini 2019-11-25

  Kikundi cha kwanza cha askari 240 wa kikosi cha 5 cha ulinzi wa amani wa China nchini Sudan Kusini wamemaliza majukumu yao ya mwaka mmoja ya kulinda amani nchini Sudan Kusini yaliyopewa na Umoja wa Mataifa na kurudi nchini China.

  • Ujenzi wa Mnara mkuu mjini Cairo unaotekelezwa na kampuni ya China waingia katika kipindi kipya 2019-11-18
  Nguzo ya chuma cha pua ya Mnara mkuu kwenye Eneo la CBD mjini Cairo, Misri unaojengwa na kampuni ya ujenzi ya China CSCEC, imewekwa tayari kwa mara ya kwanza, hatua ambayo inamaanisha kuwa ujenzi wa mnara huo unaosifiwa kama jengo refu zaidi barani Afrika umeingia katika kipindi kipya.
  • Rwanda yatafuta soko la bidhaa katika maonyesho ya pili ya CIIE 2019-11-06

  Rwanda inataka kutafuta soko la bidhaa zake katika Maonyesho ya pili ya bidhaa za kimataifa ya China CIIE na kutafuta njia ya kupanua soko la bidhaa zake nchini China. Mkuu wa idara ya uwekezaji ya bodi ya maendeleo ya Rwanda Bw. Philip Lucky, amesema Rwanda inataka kuhakikisha wateja wa China wananunua bidhaa za Rwanda na kuunga mkono mipango tofauti ya Rwanda katika kilimo na sekta nyingine.

  • Kampuni za China na Uingereza zasaini makubaliano ya awali kuongeza uwekezaji nchini Kenya 2019-11-01

  Kampuni za China nchini Kenya zimesaini makubaliano ya awali na Shirikisho la Wafanyabiashara la Uingereza tawi la Kenya (BCCK) kwa lengo la kuongeza uwekezaji katika sekta zinakazoboresha maisha ya jamii nchini humo.

  • Wanavijiji wa vijiji 1,000 nchini Nigeria waunganishwa na huduma za televisheni ya Satellite 2019-10-30

  Mradi wa "Kuunganisha vijiji elfu kumi kwa huduma za televisheni ya Satellite" nchini Nigeria umetangazwa kukamilika. Wanavijiji wa vijiji elfu moja nchini humo sasa wanaweza kuangalia televisheni ya Satellite.

  1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 next
  SearchYYMMDD  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako