• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • •  Bi.Li Chunfeng na supermarket yake ya upendo
    Bibi huyu ameshikilia kufanya shughuli za hisani kwa miaka 36, ambapo kila siku anaainisha na kugawa nguo kwa walemavu wa viungo, walemavu wa akili na watu maskini vijijini. Hadi sasa amegawa nguo zaidi ya elfu kumi.
    • Kijiji chenye wawimbaji wengi

    Kijiji cha Tongtou, mkoani Henan kinaitwa "Kijiji kinachoweza kuimba", kwani wanakijiji wake wote wanajua kuimba, karibu kila mtu anaweza kuimba nyimbo zaidi ya 100. Katika kipindi cha leo, tutazungumzia mabadiliko yaliyoletwa na uimbaji kwa maisha ya wanakijiji wa kijiji hicho.

    • Jaribio la pili la ujasiriamali kwa kijana Qi Yang
    Mwaka jana kijana Qi Yang mwenye umri wa miaka 25 alirudi katika maskani yake Zhucheng mkoani Shandong kutoka Beijing, alikofanya kazi za vibarua kwa muda wa miaka 10, na kuanzisha mkahawa wake wa chakula cha nyumbani. Mkahawa wenye mapambo ya mtindo wa kale, chakula cha kifahari na mjasiriamali kijana aliyezaliwa baada ya miaka 90, yote hayo yamekuwa ni mambo ambayo wakazi wa huko wanapenda kuyazungumzia. Kila siku mkahawa wake unajaa wateja, na hali hii pia inamtia moyo Qi Yang.
    • Bibi Zhang Rong na kahawa anayopenda
    Miaka 10 iliyopita, Bibi Zhang Rong, msichana aliyezaliwa baada ya mwaka 1980 alikuwa chuoni akisomea kozi ya biashara ya kimataifa. Wakati huo alianza kuipenda kahawa. Kwa sasa anatembelea tovuti mbalimbali za kahawa za nchini na za nchi za nje, na kubadilishana maoni kuhusu kahawa na washabiki wa kahawa kwenye mtandao wa Internet. Baada ya kuhitimu chuo kikuu, bibi Zhang Rong kwa nyakati tofauti alikwenda Shanghai na Beijing kujihusisha na kazi za kutengeneza kahawa na kutoa mafunzo kuhusu kahawa, na tabia yake ya kupenda kukaanga mbegu za kahawa mwenyewe nyumbani ikakuwa kazi yake rasmi, yaani mtengenezaji wa kahawa.
    • Mjumbe wa bunge la umma la China kwenye eneo la Shijingshan mjini Beijing Yang Guibao
    Kwa mujibu wa mpangilo wa mji, kati ya mitaa miwili ilibaki sehemu yenye urefu wa mita 350 na upana wa mita 25 kwa ajili ya kujenga barabara, lakini ilikuwa vigumu kuamua barabara hiyo inapaswa kujengwa na nani na kwa namna gani. Polepole, barabara hiyo ikasahaulika, na ikajaa takataka kila mahali.
    • Mjasiriamali kijana Zhang Chao
    Bw. Zhang Chao ni kijana aliyezaliwa mwaka 1985 hapa Beijing, sasa yeye ni mmoja wa waanzilishi wa tovuti ya Kanjia, ambayo inashguhulikia mauzo ya nyumba. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, aliwahi kuwa mtengeneza progamu za kompyuta. Mwaka 2011 alianza kujishughulisha na biashara ya nyumba. Baada ya miaka mitatu, pamoja na uzoefu wake mwenyewe wa kupanga na kununua nyumba, Bw. Zhang Chao alitambua dosari mbili kubwa kwenye biashara ya nyumba, yaani kutokuwa na taarifa sawa kati ya wauzaji na wanunuzi wa nyumba na huduma mbaya kwa wateja. Kwa hiyo mwaka 2014, Bw. Zhang Chao na marafiki zake walifikiria kuanzisha kampuni ya biashara za nyumba.
    • Maskani yetu mjini Shanghai
    Mkahawa wa Yelixiali ni mkahawa mkubwa zaidi wa kabila la Wauyghur mjini Shanghai. Kila inapofika jioni, mkahawa wa Yelixiali unafurika wateja. Si kama tu mgahawa huu una vitoweo halisi vya Xinjiang, bali pia una vitoweo vya mkoa huo vilivyotekebishwa kutokana na upendeleo wa Washanghai, na kila usiku lazima kuna nyimbo na ngoma za Xinjiang.
    • Kijiji cha kabila la Wayao mkoani Guangdong kinavyoendeleza shughuli maalum kuwasaidia wanakijiji kuondokana na umaskini
    Kijiji cha Lianshui cha wilaya inayojiendesha ya kabila la Wayao ya Liannan mjini Qingyuan mkoani Guangdong ni kijiji chenye milima mingi, na eneo dogo la ardhi isiyo na rutuba kwa ajili ya mashamba. Kabla ya mwaka 2008, kijiji hicho kilikuwa ni kijiji cha watu maskini. Lakini mwaka 2009, mkoa wa Guangdong ulianzisha kazi maalum ya kuleta maendeleo na kuondoa umaskini, na kufanya ujenzi na marekebisho ya barabara na kufanya usafi wa kijiji hicho, ambao uliboresha sura na mazingira ya kijiji hicho.
    • Kijiji kizuri cha Zhongliao mkoani Hainan China
    Kama ukienda kisiwani Hainan kusini mwa China, unaweza kusikia kuhusu kijiji kidogo lakini kizuri huko Sanya. Kijiji hicho chenye mandhari nzuri ya kupendeza kinaitwa Zhongliao, mazingira yake ni mazuri na watu wa huko wanafuata sana maadili na wanaishi kwa furaha. Wanakijiji wa kijiji hicho hawakati mti hata kidogo, na wala hawabomoi nyumba, au kujenga kuta ovyoovyo. Si waroho na wala hawafuati mitindo ya kisasa.
    • Maisha yetu ya "mikononi"
    Ni muda mfupi umepita tangu watu washerehekee sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya. Wachina wanaopenda kusherehekea sikukuu hizo, mbali na kununua vitu wanavyopenda na kula chakula kitamu, pia wana njia mpya ya kusherehekea sikukuu, yaani wanawatumia marafiki, jamaa au wapendanao bahasha nyekundu iliyowekwa pesa, lakini si ya karatasi kama zamani, bali ni ya kitarakimu kwa njia ya simu za mkononi kupitia APP ya mawasiliano Wechat.
    • Kijiji kizuri cha Wentong mjini Wanning mkoani Hainan
    Tukizungumzia mambo ya kijiji, huenda bado unayofikiria ni picha ya "takataka kila mahali na kutokuwa na utaratibu". Lakini nchini China kadiri vijiji vinavyoendelezwa, ndivyo mwamko wa wakulima kuhifadhi mazingira wanayoishi na mazingira ya asili inavyoinuka.
    • Ndoto ya waridi ya kijiji cha kabila la Wali mkoani Hainan
    Waridi ni maua yanayoota katika ukanda wenye halijoto ya wastani, kwa hiyo ni adimu kuonekana katika mkoa wa Hainan wenye halijoto ya tropiki. Baada ya kufanya majaribio ya miaka mingi, hatimaye mwaka wa 2008, wataalam wa kilimo walifanikiwa kupanda ua la kwanza la waridi mjini Sanya, na kumaliza historia ya mkoa wa Hainan kutokuwa na maua ya waridi.
    • Eneo la biashara kupitia mtandao wa internet la kijiji cha Qingyuan lasaidia kuanzisha shughuli kwenye mtandao wa internet
    Sehemu ya Qingxin ya mji wa Qingyuan, kaskazini mwa mkoa wa Guangdong China ni sehemu inayozalisha mazao ya kilimo kwa wingi. Sehemu hiyo imezungukwa na milima, na wakazi wa eneo hilo wanajihusisha na kilimo cha matunda na mboga.
    • Mradi wa uhamiaji wa Ningxia wasaidia watu wa milimani kuishi katika nyumba mpya
    Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wahui wa Ningxia uko kaskazini magharibi mwa China, na unaweza kugawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kaskazini ya mkoa huo ni tambarare, na Mto Manjano unatiririka kupita kwenye sehemu hiyo, lakini sehemu ya kusini ina milima mingi, ambayo imefunikwa na udongo wa manjano, na inapata milimita 300 za mvua kwa mwaka.
    • Mabadiliko ya Ziwa Honghu yaonesha juhudi za China kuhifadhi ardhi oevu
    "Katika ziwa la Honghu mawimbi yanapigana pigana, nyumba yangu iko kando ya ziwa. Asubuhi nakwenda kuvua ziwani, jioni narudi na samaki wengi. Bata na mayungiyungi vinaonekana ziwani, katika majira ya mpukutiko watu wanavuna mpunga mashambani."
    • China yajitahidi kujiendeleza bila ya uchafuzi
    Mwaka 1872, mbuga ya kwanza ya taifa duniani yaani Mbuga ya taifa ya Yellowstone ilianzishwa nchini Marekani. Sasa ni miaka 143 imepita, na nchi karibu 100 duniani zimeanzisha mbuga zaidi ya 600 ya taifa. Tarehe 21 Juni mwaka 2007, Mbuga ya taifa ya Pudacuo katika kata ya Shangri-la ilizinduliwa rasmi nchini China. Mwaka huu aina nyingine ya mbuga ya taifa imezinduliwa nchini China.
    • China yahamasisha "watu wote kusoma vitabu"
    Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uchumi wa China kukua kwa kasi, tabia ya kusoma vitabu imeathiriwa kutokana na mtindo wa maisha, michezo mingi ya televisheni, na matumizi ya mtandao wa internet. Kutokana na hali hiyo China ilianzisha "mradi wa kuongeza elimu" kwa kuwahamasisha wananchi wasome vitabu.
    • Mvuto wa marathon nchini China
    Mchezo wa mbio za marathon ambao kwa sasa hapa China unaonekana kushika kasi, na kuendelea kuwa moja ya michezo inayoanza kuzoeleka miongoni mwa wachina.Tukiangalia takwimu za mwaka huu tunaweza kuona kuwa idadi ya mashindano yaliyosajiliwa katika shirikisho la riadha la China ilifikia 130, ikilinganishwa na idadi hiyo ya mwaka jana ni 51. Tunaweza kusema kila wikiendi hapana China mashindano mawili ya marathon yanafanyika. Lakini siku ambayo kulikuwa na mashindano mengi zaidi ni tarehe 18 Oktoba, ambapo kulikuwa na mashindano 11.
    • Mapambano dhidi ya UKIMWI
    Tarehe 1 Desemba ni siku ya UKIMWI duniani, serikali ya China ilitoa takwimu zinaonesha kuwa kwa sasa hapa China kuna watu laki 5.75 wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Idadi hii ni sehemu ndogo sana ya idadi ya jumla ya watu zaidi ya bilioni 1.3 wa China. Na kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita kiwango hicho kimeendelea kudhibitiwa bila kuwa na ongezeko kubwa.
    • China yakabiliana changamoto za mabadiliko ya muundo wa idadi ya watu
    Katika siku za hivi karibuni, serikali ya CHina ilitangaza kufanya marekebisho ya sera ya uzazi wa mpango, inayowataka wanandoa kuwa na mtoto mmoja. Kutokana na mabadiliko hayo, wanandoa wachina sasa wanaruhusiwa kuwa na watoto wawili.kufanyiwa marekebisho kwa sera hiyo, kunatokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye jamii ya China, yaliyowalazimu watunga sera kufanya marekebisho. pamoja na kwamba China ni nchi kubwa na yenye idadi kubwa ya watu, kumekuwa na dalili za kuzeeka kwa jamii na kupungua kwa idadi ya watu wenye umri wa kufanya kazi.
    1 2 3 4 5 6 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako