• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • • Ukumbi wa maonesho ulioko katika kambi la wakimbizi wa Wapalestina
    Katika kambi ya wakimbizi iliyoko mjini Jenin, kaskazini mwa ukanda wa Mto Jordan, upo ukumbi maalum wa maonesho, ambao ulijengwa mwaka 2006 na mwigizaji, mwongozaji na mwanaharakati wa kijamii maarufu wa Israel Bw. Juliano Mer Khamis. Katika miaka 10 iliyopita, ukumbi huo unaoitwa "Uhuru" umehuhudia masikitiko na pia matumaini ya vijana na wasichana wa Palestina wanaoishi kwenye maeneo yanayokaliwa na Israel.
    • Watoto kuendelea kupata usaidizi na taasisi za fedha
    Huku idadi ya watoto maskini wenye kiu ya masomo ikiongezeka barani Afrika, mashirika mbali mbali yasiyo ya kiserikali zikiwemo taasisi za kifedha yameanza kuunga mkono jamii kwa kutoa msaada wa masomo kwa watoto hao ili kuhakikisha wanapata fursa ya kuwa na maisha mazuri katika siku za baadaye.
    • Baba anayesafari na familia yake katika sehemu mbalimbali duniani
    Inaaminika kwamba kusafiri kunaweza kupanua ufahamu wa mtu na kuweza kupata uzoefu mpya wa kina wa utamaduni wa sehemu mbalimbali, lakini imani hii pia inatumika kwa watoto?
    • Wadau wa sekta mbalimbali wana matarajio ya kuchaguliwa kwa katibu mkuu mwanamke kwa kwanza wa Umoja wa Mataifa
    Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita lilianza mchujo wa siku tatu wa wagombea wanane wa nafasi ya katibu mkuu wa Umoja huo. Wakati vyombo vingi vya habari vinafuatilia jukwaa hili lililotolewa kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja huo kwa wagombea wa nafasi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kujieleza, wadau wa sekta mbalimbali wanajadili tena ni sifa gani ambazo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anapaswa kuwa nazo na anatakiwa kubeba wajibu gani.
    • Mtunzi wa hadithi za watoto wa China ashinda tuzo ya Hans Christian Andersen
    Mtunzi wa hadithi za watoto wa China ambaye pia ni profesa wa Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Cao Wenxuan ameshinda tuzo ya Hans Christian Andersen kwa mwaka huu katika maonesho ya 53 ya Vitabu vya Watoto ya Bologna yaliyofanyika nchini Italia. Cao ni mtunzi wa kwanza kutoka China aliyeshinda tuzo hiyo ambayo ni ya ngazi ya juu zaidi kimataifa inayotolewa kwa mtunzi na mchoraji wa picha kwa ajili ya vitabu vya watoto. Huu ni wakati mwingine wa kuona fahari kwa sekta ya fasihi ya China baada ya mtunzi mwingine aitwaye Mo Yan kushinda tuzo la Noble mwaka 2012.
    • Mazoezi ya Yoga yakumbatiwa zaidi na Wachina
    Mazoezi ya yoga hivi sasa yamejipatia umaarufu mkubwa sana hapa China, na pengine kuliko hata mazoezi ya aina nyingine. Yoga ni mchanganyiko wa mazoezi ya kutafakari, vitendo, pamoja na kupumua. Lakini kwa hapa China kuna tabia ya watu wengi sana kufanya mazoezi ya yoga. Na watu hao wanafikia hadi 100.
    • Sera ya "kuwa na watoto wawili" yasaidia kuelekea uwiano wa kijinsia
    Tafiti nyingi zilizofanywa zinaonyesha kuwa wanandoa wengi nchini China, hususan kwenye maeneo ya vijijini wanaonyesha wazi kupendelea zaidi watoto wa kiume. Mamlaka ya Takwimu nchini China imesema kuwa, mpaka kufikia mwisho wa mwaka jana, idadi ya watu wanaoishi China bara ilifikia bilioni 1.37, ambao milioni 704.14 ni wanaume na milioni 670.48 ni wanawake. Hii ina maana kuwa, mamilioni ya wanaume huenda wakashindwa kufunga ndoa. Data hizo zinaonyesha kuwa, usawa wa kijinsia ni wanaume 105.0 kwa wanawake 100, na kwa watoto wanaozaliwa ni wanaume 113.51 kwa wanawake 100.
    • Pengo la kijinsia barani Afrika lapungua
    Nchi za Afrika imepiga hatua kubwa katika kupunguza pengo la kijinsia, lakini bado kuna mambo mengine kadhaa ambayo yanatakiwa kuondolewa ili kuhakikisha wanawake wanapata elimu, huduma za afya, na fursa za kiuchumi. Pengo hilo linaendelea kupungua kutokana na hatua za baadhi ya wanawake kuingia katika ulingo wa siasa pamoja na kufanya kazi. Katika bara la Afrika, Rwanda imepata mafanikio zaidi katika kujumuisha wanwake kwenye nafasi za uongozi, hususan kwenye bunge la nchi hiyo.
    • Watoto wasaidia kulinda Milu
    Hifadhi ya kitaifa ya Tian'ezhou Milu katika mkoa wa Hubei ilijengwa mwaka 1991 ili kumlinda mnyama aitwaye Milu, ambaye pia anajulikana kama Kulungu Père wa Daudi. Kwa sababu sehemu kubwa ya hifadhi hiyo iko kwenye eneo la mashamba, ni muhimu kwa wenyeji wa eneo hilo kuongeza uelewa wa jinsi ya kumtunza myama huyo.

     

    • Sera bora zaidi zinatakiwa nchini China kuunga mkono wafanyakazi wanawake wanaosomea sayansi
    Ukosefu wa usawa kwenye nyanja za sayansi, teknolojia, uhandisi, na hesabu unafuatiliwa sana nchini China katika miaka ya karibuni. Sasa kundi la wanasayansi wanawake na wahandisi wanazitaka mamlaka kutoa sera rafiki zaidi ili kuunga mkono wanawake wafanyakazi na wanafunzi wa kike wanaosomea sayansi.
    • Kutengeneza filamu ya katuni kwa Familia nchini China
    Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2015, wapenzi wa filamu nchini China walitumia zaidi ya Yuan bilioni moja na nusu kwenye filamu za katuni. Hiyo ni zaidi ya ilivyokuwa kwenye maumba ya sinema kwa muongo mmoja uliopita. Huku mahitaji ya filamu za katuni yakiongezeka nchini China, idadi ya watazamaji walio na mahitaji tofauti ya filamu za aina hiyo pia inaongezeka. Lakini sekta hii ina uwezo wa kutimiza mahitaji ya makundi mbalimbali ya watu?
    • Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika asema haki ya wanawake ni muhimu kwa maendeleo ya Afrika
    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bibi Dlamini Zuma amewataka viongozi wa nchi za Afrika kuhakikisha haki za wanawake zinaheshimu katika nchi zao. Bi Zuma amemtaja mwanamke kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya jamii na kusisitiza haja ya kuhakikisha anachukua nafasi yake katika ajenda ya maendeleo ya mwaka wa 2063. Kwa maelezo zaidi kuhusu habari hiyo huyu hapa Jacob Mogoa akiripoti kutoa Addis Ababa, Ethiopia.
    • Uchapishaji wa 3D wasaidia watoto walemavu
    Bw. Chen amefanya kazi za uchapishaji wa 3D kwa zaidi ya miaka mitatu, yeye anaendesha kampuni moja ya uchapishaji wa 3D mjini Cangzhou mkoani Hebei. Baada ya kufahamishwa kuwa mtoto mmoja aliyeko mjini Shizuishan mkoani Ningxia, zaidi ya kilomita moja kutoka mji anaoishi yeye anahitaji mkono mmoja wa kuchapishwa, alipokea kazi hiyo, kwani anaona furaha kubwa kuweza kufanya shughuli za utunzaji jamii kwa kutumia uwezo wake. Lakini kumtengenezea mkono wa bandia kwa mtoto aliyeko mbali sana siyo kazi rahisi, na vilevile hali ya ulemavu ya mtoto huyo ni maalum.
    • Kambi yenye mfumo wa kijeshi yasaidia watoto kuondokana na kupendelea kutumia mtandao wa internet
    Vijana wengi nchini China wanapendelea zaidi kutumia mtandao wa internet, na ili kukabiliana na suala hilo, kambi zenye mfumo wa kijeshi zinaanzishwa kwa wingi ili kuwasaidia kuondokana na tabia hiyo.
    • Changamoto anazokabiliana nazo mtoto mlemavu asiye na mikono Elisha Angombi
    Karibu msikilizaji kwenye kipindi hiki cha sauti ya wanawake, hiki ni kipindi kinachokuletea masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke pamoja na mtoto. Na katika kipindi cha leo tutazumngumzia mtoto mlemavu aitwaye Elisha Angombi wa nchini DRC na jinsi anavyokabilia na changamoto mbalimbali katika maisha yake ya kila siku. Zakia ana ripoti zaidi.
    • Hisia za wachina kuhusu kuondolewa kwa sera ya mtoto mmoja
    Hivi karibuni serikali ya China iliamua kufuta sheria iliyodumu kwa zaidi ya miongo mitatu iliyokuwa ikizitaka familia za nchi hii kutozaa zaidi ya mtoto mmoja. Wanandoa sasa wanaweza kuzaa watoto wawili, hatua hii ikiwa imechukuliwa ili kuepuka mwanya wa ukosefu wa nguvu kazi kwani watu wengi wanaendelea kuzeeka. Sheria hii mpya hata hivyo imepokelewa kwa hisia tofauti na raia wa China.
    • Watoto wakiwezeshwa kuwapenda wanyama pori itasaidia kupunguza ujangili katika siku zijazo
    Leo hii tutaangalia zaidi watoto wa shule nchini Kenya na fursa za kuangalia wanyama pori, kwani kama tunavyofahamu kuwa watoto ndio viongozi na walinzi wetu wa siku za baadaye, hivyo kama tukiwaandaa, kuwakukuza na kuwajengea tabia nyoofu itasaidia katika maisha yao ya baadaye.
    • Ripoti ya mwaka 2015 kuhusu pengo la kijinsia duniani
    Kongamano la uchumi duniani lililofanyika mjini Geneva hivi karibuni lilitoa Ripoti ya mwaka 2015 kuhusu pengo la kijinsia duniani, ambayo inaonesha kuwa katika miaka 10 iliyopita, pengo la jumla kati ya wanaume na wanawake duniani katika upande wa afya, elimu, nafasi za kiuchumi na nafasi za kushiriki kwenye shughuli za kisiasa limepungua kwa asilimia 4, huku pengo la kiuchumi likipungua kwa asilimia 3 tu.
    • Liang Zi kutoka china alitaka zaidi kufahamu utamaduni na desturi za Afrika

    Kwa watalii wengi wanaoenda Afrika, lengo lao kuu ni kujionea wanyama pori na kuishi katika hoteli za kitalii.

    Hivyo mara nyingi wanakosa kujumuika na jamii za kawaida barani humo na hawafahamu jinsi watu wa Afrika wanavyofanya mambo kama vile ndoa, mapishi na shughuli za kijamii.

    Lakini kwa mtalii mmoja kutoka China, Liang Zi alikuwa na lengo tofauti. Ametembeleza zaidi ya nchi saba barani Afrika na kwenye kila nchi alikwenda kuishi kwenye vijiji vidogo ambako aliishi na kulala na watu wa vijiji hivyo vingi vikiwa havina huduma na umeme ama mtandao.

    • Kampeni za wanawake wa Burundi za kuhakikisha wanaume wanakuwa bega kwa bega na wanawake katika kazi za nyumbani

    Karibu katika kipindi cha sauti ya wanawake, katika kipindi cha leo tumepata bahati ya kuongea na Meneja wa Redio na Telesheni nchini Burundi Bibi Janeth Ntiranyibagira ambaye alikuja hapa Beijing China kwenye semina ya mwezi mmoja.akiwa kama mwanamke kiongozi alieleza juhudi anazofanya ili kuhakikisha wanawake wengiwe nao wanapata wadhifa na kujikomboa kimaisha kama yeye. Pia kampeni wanazoendesha ili kuwashawishi wanaume kuwa bega kwa bega katika kasi mbalimbali hususan za nyumbani. kama kawaida mimi Pili Mwinyi na mwenzangu ni Caroline Nassoro pamoja na mgeni wetu Janeth Ntiranyibagira karibuni.

    1 2 3 4 next
    SearchYYMMDD  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako