• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Sera ya kidiplomasia ya nchi kubwa yahimiza maendeleo ya urafiki kati ya China na nchi nyingine 2018-03-08

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi, amekutana na waandishi wa habari mjini Beijing kuelezea utekelezaji wa sera ya mambo ya nje ya China katika mwaka uliopita, na mipango ya mwaka huu ya utekelezaji wa sera hiyo.

  • Bunge la China lakutana kujadili utendaji wa serikali, mageuzi ya katiba 2018-03-08
  Mikutano miwili mikubwa ya mwaka, yaani Baraza la mashauriano ya Kisiasa, na bunge la umma la China, inafanyika. Hii ni mikutano ya uwakilishi wa wananchi, ambayo wajumbe wake wanawakilisha maoni ya wananchi kwa chama na serikali.
  • Internet yawa moja ya maeneo ambayo ni fursa ya maendeleo kwa watumiaji 2016-11-16
  Mkutano kuhusu maendeleo ya internet duniani umefunguliwa leo katika mji wa Wuzhen, Mkoani Zhejiang kusini mwa China. Mkutano huu wa kila mwaka unafanyika wakati China inapata maendeleo ya kasi kwenye teknolojia ya mawasiliano na habari, na inashirikiana na nchi mbalimbali za Afrika kupiga hatua kwenye eneo hilo.
  • Internet yawa moja ya maeneo ambayo ni fursa ya maendeleo kwa watumiaji 2016-11-16

  Mkutano kuhusu maendeleo ya internet duniani umefunguliwa leo katika mji wa Wuzhen, Mkoani Zhejiang kusini mwa China. Mkutano huu wa kila mwaka unafanyika wakati China inapata maendeleo ya kasi kwenye teknolojia ya mawasiliano na habari, na inashirikiana na nchi mbalimbali za Afrika kupiga hatua kwenye eneo hilo. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni "Uvumbuzi unaoeleta maendeleo ya kunufaisha wote – kujenga jamii yenye mustakbali wa pamoja kwenye mtandao wa internet ".

  • Mafanikio na Changamoto mpya za Sera ya Mtoto mmoja wa China 2016-11-15

  KWA muda wa zaidi ya miaka 35 sasa nchi ya China imekuwa inafuata Sera ya Mtoto mmoja, sera ambayo lengo lake kubwa ni kudhibiti ongezeko kubwa la idadi ya watu, ambalo China iliona kuwa ni changamoto kwa familia na kwa serikali. Mwanzoni wakati sera hii inaanza kutekelezwa kulikuwa na maswali kama kweli itakuwa na ufanisi na kama kweli inaendana na utamaduni wa wachina.

  • Sekta ya Elimu: Tukumbuke elimu ni zaidi ya kufuta ujinga 2016-11-15

  Kwa muda mrefu sasa kila maadhimisho ya siku ya elimu yanapokaribia, tumekuwa na desturi ya kujadili maendeleo ya elimu kwa kuangalia kigezo cha watu wanaojua kusoma na kuandika. Tunaangalia takwimu hizo kwa kuwa zamani hasa kipindi baada ya uhuru, hicho kilikuwa moja ya vigezo muhimu vya kuangalia maendeleo ya elimu. Lakini kwenye karne hii tunayoita karne ya sayansi na teknolojia, kuna mengi sana tunayotakiwa kuyatumia kama vigezo vya kupima maendeleo ya elimu. Kuna baadhi ya vigezo tumefanya vizuri, kuna baadhi ya vigezo tunajikongoja na kwenye vigezo vingine bado tuko nyuma sana.

  • Soko la China, fursa iliyo wazi kwa watanzania tunayoichezea 2016-11-15

  Mwezi Julai mwaka jana serikali ya Tanzania ilituma ujumbe mkubwa wa kiutendaji hapa Beijing China, uliokusanya watu kutoka wizara, idara, makampuni, jumuiya na taasisi mbalimbali za Tanzania, ukiwa na lengo la kutafuta fursa za biashara kwa ajili ya Tanzania na watanzania. Kwenye mkutano huo wa mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), lengo kubwa lilikuwa viongozi wa kisiasa kuangalia maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na viongozi wengine watendaji walikuwa wakiangalia ni vipi wataweza kupata fursa zenyewe na kuzitumia. Kwenye mkutano huo kuna mambo mawili makubwa niliyoyaona, moja la kufurahisha na lingine la kusikitisha.

  • Mpango wa China kuvutia Wataalam, Tanzania tuanze kuthamini wa kwetu 2016-11-15

  SIKU chache zilizopita nilibahatia kuhudhuria mkutano kati ya Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang na wataalamu kutoka nje wanaofanya kazi hapa China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako