• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • • Wasomi na mikakati ya China kumaliza umasikini Afrika 2017-06-20

  AFRIKA yenye idadi ya watu zaidi ya bilioni 1.1 ina rasilimali nyingi za asili zenye thamani kama Mafuta, gesi, madini mbalimbali na vinginevyo lakini inakabiwa na changamoto kubwa ya umasikini. Wasomi wa China na Afrika walikutana mwaka jana nchini China na kuzungumzia sababu za Afrika kukithiri kwa umasikini na mikakati ya kupunguza umasikini. Inakadiliwa kuwa asilimia 75 ya nchi masikini duniani ziko katika bara la Afrika. Hali ya Umasikini:

  • Mafanikio na uzoefu wa China katika kupunguza umaskini 2017-06-20

  "LAZIMA tuondoe umaskini ambao upo katika akili zetu kabla ya kuuondoa ndani ya maeneo tunaotawala, kabla ya kusaidia raia na taifa kutoka kwenye minyororo ya umaskini na kuanza barabara ya mafanikio." Haya ni maneno ya kiongozi wa China Xi Jinping katika kitabu chake maarufu "Kuondokana na Umaskini." Kitabu hiki kinatoa maelezo ya kina kuhusu jinsi yeye alifanikiwa kukabiliana na kushinda vita dhidi ya umaskini kama kiongozi katika Ningde, moja ya sehemu ya Mkoa wa Fujian iliyokuwa na umaskini zaidi katika miaka ya 1980.

  • Mkoa wa Qinghai wazingatia kuboresha maisha ya watu na kuondoa umaskini 2017-06-08

  Mkoa wa Qinghai liko uwanda wa juu magharibi mwa China. Hali ya maendeleo ya mkoa huo inakabiliwa na changamoto nyingi. Asilimia 90 ya watu maskini wanaishi katika eneo la milimani au maeneo yenye ukame. Ni vigumu kuwasaidia watu wa huko kuondokana na umaskini kutokana na maafa mengi, na kuwa na msingi dhaifu wa uchumi.

  • Bw. Luo Junyuan kusaidia watu wa mji wa Jing Gangshan kuondoa umaskini 2017-06-06

  Mji wa Jing Gangshan uko katika eneo la mlima wa Luoxiao ambalo kati ya mkoa wa Jiangxi na Hunan. Ni mji wenye rasilimali nyingi za wanyama, miti na una hali ya hewa nzuri. Lakini kutokana na mji huo kuwa katika eneo la milimani, maendeleo yake yameathiriwa. Eneo hilo lilikuwa eneo la maskini zaidi nchini China kutokana na matatizo ya usafiri, na msingi dhaifu wa uchumi. Fadhili Mpunji na maelezo zaidi kuhusu juhudu za mji huo kuondokana na umaskini.

  • Kijiji cha Maerzhuang chatajirika kutokana na ufugaji wa kondoo 2017-05-25

  Kwenye tafrija ya kuwakaribisha viongozi waliohudhuria mkutano wa kundi la nchi 20 (G20) uliofanyika mwaka jana huko Hangzhou, chakula kimoja cha nyama ya kondoo kilikaribishwa na viongozi wengi. Kondoo hao ni kutoka wilaya ya Yanchi mkoani Ningxia, China. Mwandishi wetu wa habari alipofanya mahojiano kwenye wilaya hiyo, ameona kuwa kondoo wa huko wanafugwa kwenye mashamba yenye mazingira asili, na wakati fulani wanaweza kusikiliza muziki. Hivi sasa wakulima wengi wa huko wametajirika kutokana na ufugaji wa kondoo.

  • Uuzaji wa vifaa vya jukwaani vilivyotengenezwa na kijiji cha Huozhuang mkoani Henan vyanufaika na maendeleo ya mtandao wa Internet 2017-05-22
  "Shehuo" ni shughuli za burudani kwa wachina kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa Kichina, ikiwemo ngoma ya simba, na ngoma ya dragon. Utengenezaji wa vifaa vya jukwaani vya Shehuo katika kijiji cha Huozhuang mkoani Henan nchini China una historia ya miaka zaidi ya 100. Zamani wanakijiji walitengenza vifaa hivi katika karahana ndogo na mauzo ya vifaa hivi yalikabiliwa na changamoto nyingi.
  • Mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza umaskini katika miaka ya hivi karibuni nchini China 2017-05-18

  Umaskini ni tatizo kubwa linalokabili dunia nzima. Takwimu zilizotolewa mwaka 2016 na Benki ya Dunia zimeonesha kuwa, hivi sasa duniani kuna watu maskini milioni 700. China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea, ingawa idadi ya watu wake maskini imepungua kutoka milioni 82 ya mwaka 2012 hadi milioni 40 ya hivi sasa, lakini lengo la serikali ya China ni kutokomeza kabisa tatizo la umaskini kabla ya mwaka 2020. Ili kutimiza lengo hilo, rais Xi Jinping wa China imeagiza kuchukua hatua halisi zenye ufanisi kuhusu suala hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako