• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zoezi la kukusanya picha kwa ajili ya maadhimisho ya "miaka 55 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania"

  (GMT+08:00) 2019-02-25 08:55:46

  Mwaka huu China na Tanzania zinaadhimisha miaka 55 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi. Ili kuadhimisha na kudumisha urafiki wa jadi kati ya nchi hizi mbili, Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China imeandaa shindano la kukusanya picha kwa ajili ya maadhimisho hayo.

  A. Tunachohitaji

  Picha zinazoonesha urafiki kati ya Tanzania na China, zinazoonesha matukio na mafanikio ya ushirikiano katika miaka 55 iliyopita, kusaidiana kati ya wachina na watanzania, na maisha ya kawaida yanayohusu nchi hizo mbili.

  B.Wanaostahili kushiriki

  Wasikilizaji wetu wote wa Afrika Mashariki.

  C. Jinsi ya kushiriki

  i). Tuma picha uliyopiga na hakikisha una hakimiliki ya picha hiyo.

  ii). Weka maelezo yenye maneno kati ya 100 na 200 kuhusu picha hiyo.

  iii). Andika jina lako kamili, njia ya mawasiliano na picha yako.

  D. Njia ya kutuma picha na maelezo yako

  i). Tuma kwa njia ya baruapepe kwa anuani yetu ya kiswahili@cri.com.cn

  ii). Andika "Uhusiano kati ya China na Tanzania" kwenye kichwa cha baruapepe yako.

  iii). Mwisho wa kutuma picha ni tarehe 31 Machi.

  E. Washindi

  Picha zitazokidhi vigezo vyetu zitawekwa kwenye tovuti zetu za swahili.cri.cn na facebook.com/kiswahilicri. Kadiri picha hizo zitakavyoenezwa kwenye ukurasa wetu wa facebook itakuwa ni kigezo muhimu tathmini ya thamani ya picha, na kiwango cha kukubalika kwa na maoni yatakayotolewa pia kitatiliwa maanani. Mwisho tathmini itakuwa tarehe 25 Aprili, na matokeo yatatangazwa tarehe 26, Aprili.

  F. Tuzo

  Mshindi mmoja wa nafasi ya kwanza atapata zawadi yenye thamani ya dola 200 za kimarekani.

  Washindi watano wa nafasi ya pili watapata zawadi yenye thamani ya dola 100 za kimarekani.

  Washindi kumi wa nafasi ya tatu watapata zawadi yenye thamani ya dola 50 za kimarekani.

  Usikose fursa hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako