• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikutano ya baraza la diplomasia ya umma kufanyika tarehe 9 mjini Dar es Salaam

    (GMT+08:00) 2016-08-08 16:42:53
    Ili kutekeleza matokeo yaliyotimizwa kwenye mkutano wa wakuu wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka jana huko Johannesburg, Afrika Kusini, Shirika la Diplomasia ya Umma la China likishirikiana na Radio China Kimataifa litafanya mikutano ya baraza la diplomasia ya umma mjini Dar es Salaam, Tanzania tarehe 9 Agosti. Kauli mbiu ya baraza hili ni "kushirikiana, kupata mafanikio na maendeleo kwa pamoja, kusukuma mbele uhusiano na ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Afrika katika pande zote." Baraza hili litakuwa na mikutano mitatu, ikiwemo mkutano wa mawasiliano ya kiutamaduni na ushirikiano wa vyombo vya habari, mkutano wa mawasiliano na ushirikiano kwa maslahi ya umma, na mkutano wa ushirikiano wa mambo ya afya na maingiliano ya dawa za kienyeji. Wajumbe wa idara za kisiasa na kiuchumi, vyombo vya habari, idara za kitaaluma na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka China, Tanzania, Afrika Kusini, Ethiopia, Namibia, Kenya na Nigeria watafanya majadiliano kwenye mikutano hiyo. Baraza hili linalenga kuimarisha maelewano na urafiki na kusukuma mbele ushirikiano kati ya China na Afrika.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako