• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina wakaribisha majira ya machipuko kwa maadhimisho

    (GMT+08:00) 2017-04-04 15:56:48

    Na Eric Biegon, Beijing China

    Mwanzo wa Aprili inadhihirisha mwisho wa majira ya baridi, lakini la muhimu zaidi ni kwamba inatoa fursa kwa msimu mpya wa majira ya machipuko, ambalo ni tukio la kihistoria kwa idadi kubwa ya mataifa duniani.

    Kubadilika kwa misimu ina maana kubwa zaidi kwa raia wa China. Kamwe hao hawakuchukulii nguvu ya msimu mpya kwa mzaha. Ni likizo ambalo kwamba sherehe uandaliwa kwa njia ya kipekee.

    Umuhimu huu ni wa kushangaza kwani kulingana na tamaduni za Wachina, majira ya machipuko ni moja inayotunuku baraka na heri njema. Kwao ni wakati wa kuzaliwa upya. Kote nchini, anga la furaha ya msimu huu ni dhahiri.

    Ni wazi kuwa China kwa sasa, hatua kwa hatua, imeanza kupokea idadi kubwa ya wageni, wengi wao wakiwa watalii, kama mimi nilivyogundua wakati wa ziara yangu ya makavazi ya kitaifa ya China siku chache zilizopita.

    Pita pita kwa barabara kuu na mitaa ya Beijing inasimulia hali halisia kwani idadi kubwa ya watu ambao wamekuwa hawapo siku chache zilizopita sasa wamerejea. Kipindi hiki hakika kimefanya uganga wake.

    Anga ya kijivu na baridi kali

    Siku ya kwanza ya msimu huu kwa kawaida inaadhimishwa kwa sherere. Idadi kubwa ya wale ambao wanafuatilia utamaduni huu wanaamini kuwa majira haya ya machipuko hautilii kikomo msimu wa baridi pekee. Kwao mlango wa vizia ambao labda ungewatembelea ndani ya miezi michache zilizopita umefungwa.

    "Winta kwetu kunamaanisha kulala. Shughuli iko kiwango cha chini. Ni wakati wa mwanga mdogo. Maua kukauka. Watu kukaa ndani ya nyumba zaidi ya kawaida. "Mmoja wao aliniambia.

    Ziara yangu mjini Beijing ilinitunuku fursa nzuri ya kushuhudia jinsi Wachina wanavyoukaribisha msimu huu mpya. Baada ya yote niliyoshuhudia, lazima niseme sikuweza kuona kwa nini kule kubadilika kwa misimu hauwezi kusherehekewa. Kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu, baridi nyingi na anga za kijivu zimeondoka. Watu hatimaye wanafurahia mwanga wa jua zaidi, huku maua na nyasi zikichanua.

    Jumapili, nilialikwa kuhudhuria sherehe zilizoandaliwa katika bustani la Willow. Hifadhi hii ni hasa maarufu kwa mierebi nzuri, na ni hifadhi pekee Beijing ambayo ina mandhari ya vijijini. Mamia ya wakazi wa China walijumuika hapa kwa tamasha kukaribisha msimu mpya. Mwerebi ni mti ambao una historia ndefu kwa watu wa China.

    Idadi kubwa ya wale waliohudhuria, hasa wale ambao mimi nilizungumza nao, walisema kuwa mti huu unaashiria unyenyekevu na matumaini, na hii ndio sababu kuu ya kukusanyika hapa.

    Muda mfupi baadaye sherehe ikaanza. Nyimbo, ngoma na mashairi zikafuata kwa mfululizo. Vijana na wazee waliwakilishwa katika kikao hiki.

    Vazi la kale la Kichina la kitamaduni

    Idadi kubwa ya wageni waliohudhuria sherehe hizo hawakuwachwa nyuma. Wote walivishwa mavazi ya kale ya kitamaduni ya kichina. Mavazi haya kwa kawaida zilivaliwa na baba zao kusherehekea ujio wa majira ya machipuko. Mimi pia nilipata "Hanfu" yangu kama inavyojulikana kwa wachina. Hakuna hata mmoja aliyejihisi kutengwa katika maadhimisho hayo.

    Wakati wa maadhimisho hayo, nilimuuliza mmoja wa wenyeji, Bi Kelly Chen Linging, ambaye pia ni mwalimu wa lugha ya Kichina na utamaduni, kwa nini msimu huu ukasherehekewa kwa mbwembwe.

    "Katika utamaduni wetu, Majira ya machipuko ni kama msimu wa kwanza wa mwaka. Kwetu ni kama mwanzo wa mwaka. Mwanzo mpya. Basi iwapo kwa mfano tutafurahi wakati wa majira haya, kuna uwezekano mkubwa kwamba tutafurahi mwaka mzima." Bi Chen alinijibu

    Uhusiano wake na Pasaka ya Wakristo

    Wakristo kote duniani, wanaidhimosha siku kuu ya pasaka wakati wa kipindi hiki. Kwa mara nyingi, wanafunzi wanakuwa likizo nyumbani kwa mapumziko. Likizo hii iko mahali popote kati ya katikati ya mwezi wa Machi na mwishoni mwa Aprili katika kalenda ya Gregory.

    Sawia na utamaduni huu wa Kikristo, raia wa China hupata likizo ya umma ya siku tatu ya kusherehekea ujio wa majira ya machipuko. Hakuna hata mmoja anayekosa nafasi ya kuadhimisha sherehe hii.

    "Kila kitu inageuka kijani wakati wa majira haya. Ina maana ya nguvu na uwezo. upepo ni joto. nyasi uamka. Kila kitu inaamka. Kwa mara nyingine tunafuraha na amani na kila mtu anataka kusherehekea."Akasema Bi Chen

    Katika kilele cha tamasha hilo, wote waliokuwemo walipanda mti mmoja baada ya mwingine. Afrika najua kupanda miti imehusishwa sana na matukio muhimu. Lakini mimi nilitaka kubaini kwa nini Wachina wakapanda mti huo.

    "Sisi tunapanda mti kwa sababu tunatarajia itakua. Hakika itakuwa mti mkubwa. Hii ni onyesho la ukuaji kwetu. Tunatarajia kukua katika kila nyanja ya maisha yetu kuanzia msimu huu kuendelea." Bi Chen alibainisha.

    Tamasha la Qing-Ming

    Tamasha hili hata hivyo haijatia kikomo kwani ndio mwanzo tu. Siku zinazofuata bado kuna shughuli kamili. Tamasha la Qing-Ming huzingatiwa wakati wa msimu huu. Huu ndio wakati wa ufagiaji wa makaburi. Wakati wa sherehe hiyo, Wachina wanatembelea makaburi na kutoa sala kwa mababu zao. Wao hufagia makaburi na kutoa chakula kwa mababu zao. Ni wakati wa kuwaheshimu na kuwakumbuka.

    Kwa mujibu wa Bi Chen hii ndio "mwezi wa kusafisha. Ni wakati wa kuondoa mambo na vitu visinyohitajika. Aidha ni wakati wa kuhakikisha kila kitu iko katika hali nzuri."

    Mnato huu mkubwa kwa mila hii unaweza kufupishwa kwa maneno machache kutoka bwana Zhao Yongsheng, mwanachuo maarufu katika utamaduni, aliyosema wakati wa hafla ya ufunguzi ili kukaribisha msimu huu.

    "Utamaduni mufti unahitaji urithi. Tushikilie kalamu sana kufufua umaarufu wa kuandika kwa njia ya Kichina, kuimarisha kujiamini, kuboresha nguvu ya kitamaduni ya kitaifa, na kutoa msaada wa nguvu za kiroho kwa mwamko mpya wa taifa la China." Yeye alisema.

    Kwa mara nyingine tena, hii inaonyesha uaminifu wa watu wa China kwa mila zao za karne kwa karne. Makabila 56 nchini China wanasherehekea utamaduni huu kama njia ya kuonyesha heshima kwa mababu. Hivi sasa nchi ya Wachina ni dhabiti ulimwenguni kiuchumi, lakini kamwe hawajasahau walikotoka. Mafanikio yao imetokana na utamaduni huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako