• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushawishi wa Kiuchumi unaonawiri wa Mkoa wa Guangdong kwa Mataifa ya Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-05 14:22:55
    Na Eric Biegon, Guangzhou

    China imebarikiwa na kanda maalum ambayo imeiweka kwenye kilele cha uchumi duniani. Lakini jimbo la Guangdong kwa wepesi yaonekana kama kichocheo kikuu cha ushawishi wake.

    Hii ni jimbo la watu milioni 110, na yenye GDP ya trilioni 1.2 dola za Kimarekani. Ni barabara ya zamani ya biashara kutoka China kuelekea nchi za nje zikiwemo mataifa ya Afrika. Ama kwa kweli ni mkoa unaojivunia kikosi kikubwa kutoka Afrika kinachofanya biashara nchini China.

    Ni inajivunia miji mikubwa ya kibiashara duniani kama vile Guangzhou, Shenzhen, Dongguan, Zhuhai na Shantou. Haya ni maeneo maalum ya kiuchumi ambapo mipango mbalimbali ya serikali huvutia uwekezaji. Makampuni makubwa kama vile Huawei, Tencent, Hujian Group, BYD, Kampuni ya Droni ya DJI, miongoni mwa nyingine, ziko na mizizi hapa.

    Kwamba China imeongeza ushirikiano wake na nchi zinazoendelea za Afrika si siri. Hata hivyo yaonekana kuwa Mkoa wa Guangdong inachukua sehemu kubwa ya uwekezaji wa China kwa bara la Afrika.

    Takwimu Muhimu

    Mwishoni wa mwaka 2015, Uwekezaji kwa mataifa ya nje kutoka China moja kwa moja na Afrika ilifikia billioni 2.89 dola za Kimarekani. Hii ikiwa ni asilimia mbili (2%) ya jumla ya FDI kutoka China.

    Mwaka 2015, China ilikuwa imeanzisha jumla ya makampuni 3000 barani Afrika. Makampuni haya yametawanyika kaya tika mataifa Kenya, Tanzania, Ethiopia, Afrika ya Kusini, DRC, Nigeria, Zambia, Sudan, Zimbabwe, Ghana, Mauritius na Angola.

    "Afrika ni soko kubwa ya kigeni kwa China kwa miradi ya mkataba. Uwekezaji katika Afrika katika miradi hiyo imekuwa ikipanda juu kwa muda sasa. "Alibainisha Bi Wen Xiaohuan, ambaye ni naibu mkurugenzi wa kitengo cha Uwekezaji katika idara ya Biashara Guangdong.

    Takwimu katika wizara ya mambo ya nje ya China zilibaini kuwa mikataba zilizotiwa saini mpya ni kiasi jumla ya Billioni 82 dola za Kimarekani. Kiasi cha biashara ambacho kimekamilika kufikia sasa inasimamia Billioni 52.1 Dola za Marekani.

    Katika ripoti zilizotolewa na viongozi wa utawala wa Mkoa huo, Guangdong iliagiza na kuuza bidhaa Afrika kwa jumla ya Billioni 34.8 Dola za Marekani kufikia mwaka 2016, hii ikiwa ni asilimia 23.4 ya jumla ya bishara kati ya China na Afrika. Bidhaa kutoka Guangdong kuelekea Afrika ilitimu Billioni 25.5 Dola za Marekani, hii ikiwa ni asilimia 27 ya jumla ya bidhaa zilizouzwa kwa mataifa ya nje.

    "Afrika ni eneo muhimu ya makampuni ya Guangdong. Afrika ni soko tayari kwa bidhaa zinazotengenezwa kutoka Guangdong. "Xiaohuan alisema

    Uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika kuelekea mkoa huo ulifika Billioni 10.8 Dola za Marekani, ambayo ni asilimia 19 ya bidhaa zilizoagizwa China kutoka Afrika.

    Mwishoni wa 2016, Masoko ya biashara 10 kubwa kwa Guangdong katika bara la Afrika yalikuwa Kenya, Tanzania, Misri, Algeria, Morocco, Ethiopia, Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, na Angola. Bi Xiaohuan anasema nchi hizi kumi zimechukua asilimia 20 ya biashara kati ya Guangdong na Afrika.

    Guangdong imesajili miradi 1,593 ya uwekezaji kutoka Afrika na uwekezaji jumla ya Billioni 4.03 dola za Kimarekani. Mwisho wa mwaka jana, makampuni ya Guangdong zilianzisha jumla ya biashara 124 katika Afrika na jumla ya Billioni 2.31 dola za Kimarekani. Hii ikiwa ni asilimia 3.71% ya kiasi jumla ya FDI ya mkoa wa Guangdong.

    Mkoa huo kufikia sasa imewekeza sana katika Afrika katika miradi miwili. Hasa, Guangdong imeanzisha miradi ya nguvu za umeme ya Shenzhen nchini Ghana kwa jumla ya Billioni 790 dola za Kimarekani. Hii ni kwa mbali mradi mkubwa kutoka katika jimbo hilo kuelekea Afrika.

    Mradi mwingine ni ile inayofanywa na kamputi ya nishati ya Guangzhou Dongsong katika Uganda. Hii kampuni ya Kichina imeanzisha mradi wa kujenga kiwanda cha mbolea cha Sukulu. Huu ni mradi mkubwa zaidi uliofadhiliwa kibinafsi katika sekta ya madini kuwahi kufanyika Afrika. Inatarajiwa kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha wa tani 300,000 ya mbolea kila mwaka.

    Viwanda

    Wakihutubia kundi la waandishi wa habari kutoka Afrika waliokuwa kwenye ziara ya mkoa huo, maafisa kutoka wizara ya biashara ya China walibainisha kwamba Guangdong imeanzisha uwekezaji wa viwanda katika nchini ya Kenya, Uganda, Ethiopia na Nigeria.

    Jumla ya uwekezaji katika sekta hii inalenga billioni 3.7 Dola za Marekani. Maafisa hao walisema uwekezaji umeongezeka katika Afrika kwa sababu ya utulivu wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi.

    Hata hivyo hizi si sehemu tu za ushirikiano. Ripoti inaonyesha kwamba sekta ya utalii imeshuhudia maendeleo ya haraka kati ya Guangdong na Afrika

    "Tangu mwaka 2013, kumekuwa na ongezeko la watalii kutoka Guangdong ambao walitembelea mbuga mbalimbali barani Afrika. Mkoa wetu unajivunia watalii milioni 8 ambao husafiri kwa maeneo yote ya dunia kila mwaka. "Alisema bwana Luo Jun, ambaye ni naibu mkuu wa masuala ya nje ya Guangdong.

    Katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano kati ya Afrika na China imekuwa ikikuzwa kwa njia mbalimbali. Njia kubwa iliyozinduliwa hivi karibuni ni mradi wa "Invest in Africa Forum", ambayo inasukuma ushirikiano katika maeneo ya kilimo, fedha, utalii na madini uchimbaji.

    Eneo lingine ni kuanzisha mradi wa miji pacha kati ya Afrika na China. Hii iliundwa kushughulikia namna ambayo miji ya Kichina na ya Afrika yanaweza kushirikiana kwenye maendeleo ya kiuchumi na kumaliza umaskini mijini.

    Kwa mujibu wa maafisa wa Kichina, Guangdong na Afrika zinapiga hatua muhimu za kuboresha uchumi na marekebisho. Wao wamedumisha kwamba ni sahihi kwa pande hizi mbili kuungana mikono na kuendeleza ushirikiano wao katika sekta muhimu za viwanda, nishati na miundo mbinu, utalii, kilimo na masoko ya utamaduni kwa manufaa ya watu wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako