• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China kuunda Matrekta Tanzania kukuza kilimo cha Kisasa

    (GMT+08:00) 2017-06-06 16:38:27
    Na Theopista Nsanzugwanko, CHANGZHOU

    KILIMO ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi ya Tanzania, kama zilivyo nchi nyingi za bara hilo la Afrika kilimo kimekuwa kikichangia maendeleo ya uchumi kwa nusu ya pato la Taifa. Tanzania ni moja ya nchi ambazo wananchi wake walio wengi hutegemea kilimo kuendesha maisha yao ya kila siku hasa waliopo vijijini,ambapo asilimia 75 ya wananchi wote ni wakulima.

    Licha ya kuwa kilimo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya nchi bado ndiyo inayoongoza kuwa na watu wenye umasikini wa kutisha kutokana na kutumia teknolojia duni katika kilimo,hivyo kumfanya mkulima kutokuwa na maendeleo.

    Wakulima walio wengi hutumia Teknolojia duni za Kilimo ambalo ni jembe la Mkono ambalo ni vigumu kulima kilimo chenye tija. Lakini kumekuwa na Teknolojia mbalimbali za kisasa zenye uwezo wa kuboresha kukuza kilimo hivyo serikali kwa sasa imeweka mikakati ya kuhakikisha wanainua maisha ya wananchi hao wakulima kwa kuwapatia zana na kisasa.

    Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa pamoja na mambo mengine,Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa kushirikiana na kampuni ya CHANGZHOU Machine & Equipment Imp & Exp Company Limited (AMECCO) ya nchini China imeklubaliana kuanza kuweka mikakati ya kuwekeza nchini Tanzania katika kuunganisha Matrekta kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata zana hizo za kisasa za kilimo kwa bei nafuu.

    Pia kwa kutumia ushirikiano huo, unaojikita katika utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda mmoja na Njia Moja" lililoasisiwa na Rais wa China Xi Jinping mwaka 2013 kwa lengo la kuhamasisha ushirikiano baina ya Afrika na China.

    Katika Pendekezo hilo mbali na ujenzi wa miundombinu itakayosaidia katika kufanya biashara na usafirishaji wa bidhaa mbalimba pia kuna suala la ujenzi wa viwanda kwa kampuni za China kuwekeza maeneo mbalimbali Duniani.

    Kampuni hiyo ya nchini China itatoa mafunzo kwa watanzania wengi kufahamu jinsi ya kuunga na kufanyia ukarabati wake hivyo kuongeza Ajira,suala ambalo litakuwa ni kujikita katika Pendekezo hilo kwa kuhamasisha mahusiano baina ya watu kutoka pande hizo mbili.

    Makamu wa Maneja Mkuu wa Kampuni ya Changzhou AMMECO, Zhou Yongqi anasema wako tayari kwa ajili ya ushirikiano wa kuuza vipande vya matrekta na kuunganishwa nchini Tanzania. Anasema tangu mwaka 2014 walikuwa wameishakubalina na SUMA JKT kuingiza vipande vya kuunganisha matrekta 1000 lakini utekelezaji wake haukufanyika.

    Kutokana na Changamoto ya utekelezaji wa Mkataba huo, Mkurugenzi wa Utafiti,Mipango na Maendeleo ya Viwanda katika Shirika hilo, Godwill Wanga anasema kampuni hiyo inayotengeneza Matrekta nchini China itasaidia katika kuimarisha kilimo nchini. Anasema kwa sasa shirika hilo lina vipande vya Matrekta 2400 ambavyo wameanza kuunganisha matrekta 15 nchini walivyonunua toka nchi ya Polland.

    "Uhitaji wa Matrekta ni mkubwa na sasa na tumeanza kuunganisha katika eneo moja la Kibaha tu lakini kwa ushirikiano huu tutakuwa na vituo vingine Tanga, Mbeya na Mwanza ili kuweza kuwafikia wakulima wengi wa Tanzania" anasema.

    Anasema kampuni hiyo kwa kushirikiana na NDC watauza matrekta kwa wakulima na kutoa mafunzo kwa watanzania ili kukabiliana na uhaba wa watu wanaojua kutengeneza na kuunganisha Matrekta nchini.

    Kutokana na mafunzo hayo, watu watapata ajira na baada ya kuunganishwa mengi bei ya kununua itashuka na kilimo kuwa chenye urahisi hivyo kufikia lengo la serikali ya awamu ya tano ya viwanda kwa kupata malighafi za viwandani.

    Wanga anaeleza kuwa mradi huo wa matrekta wenye thamani ya dola za Marekani milioni 55 uliokuwa ukitekelezwa na SUMA JKT lakini serikali ikaamua kuhamishia NDC na kuanza utekelezaji wake Agosti mwaka jana na tayari wameunganisha Matrektor 15. Anasema kwa kutumia fedha hiyo ya mradi,pia watakuwa na vituo vya kuhudumia matrekta hayo yakiwa katika mashamba ya wakulima ili kusaidia katika uendeshaji wake na kwa sasa wana vituo nane.

    "Lakini kutokana na umuhimu wa vituo hivi,baadaye tutaongeza vingine katika maeneo yatakayokuwa yamenunua matrekta kwa wingi,na katika vituo hivyo kutakuwa na magari yenye vifaa mbalimbali kwa ajili ya kutengeneza Matrekto yatakayokuwa pamoja na fundi"anaeleza

    Anasema tofauti ya Matrekta hayo na mengine yanazingatia ubora wa viwango vya kimataifa kwani yapo amnbayo yametengenezwa kwa ubora tofauti hivyo kutomuwezesha mkulima kutumia kwa muda nrefu lakini wanayounganisha wao yatamuwezesha mkulima kutumia zaidi ya miaka 15 hadi 20.

    Wanga anasema matrekta yatakayounganishwa nchini Tanzania yatakuwa imara kwa mkulima kutumia kwa miaka 15 hadi 20 na kumsaidia mkulima kuondokana na changamoto ya kununua Matrekta nje ya nchi. Anasema mkulima atakuwa na uhakika wa matengenezo kutokana na kuwepo vituo mikoani ambapo mafundi watafuata wakulima shambani huko huko kutengeneza hivyo kupunguza gharama kwa mkulima huku yakifanyiwa ukarabati wa mara kwa mara.

    Kampuni ya AMECCO ilianzishwa mwaka 1983 na kutengeneza mashine mbalimbali huku wakishirikiana na kampuni kutoka pande zote za dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako