• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watanzania wanaokamatwa kwa Mihadarati China wapungua

  (GMT+08:00) 2017-10-11 16:22:45

  Na Theopista Nsanzugwanko, Beijing

  IDADI ya watanzania waliokamatwa kwa kuhusika na biashara ya mihadarati kutoka nchini Tanzania au ndani ya China imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka zaidi ya 30 mwaka 2013 hadi wanne mwaka huu huku mwaka jana kukiwa hakuna aliyekamatwa.

  Aidha, watanzania wanne waliokamatwa na dawa hizo nchini China ni wanaosafirisha ndani ya nchi na siyo kutoka Tanzania huku kukiwa na wafungwa 217 waliofungwa katika magereza mbalimbali huku asilimia 90 wakiwa wamefungwa kwa kujihusisha na biashara ya mihadarati.

  Hatua hiyo ,imetokana na mikakati mbalimbali ya serikali ya awamu ya tano na ile ya awamu ya nne kwani mpaka kufikia mwezi Septemba mwaka huu ni Watanzania 217 wamefungwa gerezani nchini China lakini hakuna aliyehukumiwa kunyongwa.

  Taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini China zinaeleza kuwa wafungwa hao ni kutokana na makosa mbalimbali lakini wengi wao wakikamatwa kwa kuhusiana biashara hiyo ya mihadarati kusafirisha kutoka Tanzania,ndani ya China kutoka mji wa Guangzhou kwenda Beijing na wengine kuuza ndani ya nchi hiyo.

  Balozi wa Tanzania nchini China,Mbelwa Kairuki anaeleza kuwa mwaka huu ni watanzania wanne tu walikamatwa na dawa hizo wote katika mji wa Guangzhou ambao walikamatwa kuanzia mwezi Januari hadi April kwa kuuza dawa ndani ya nchi.

  Lakini hakuna aliyekamtwa kutoa Tanzania hivyo kusaidia kudhibiti nchi kuonekana ni sehemu ya kusafirishia dawa.

  Anasema watanzania waliofugwa nchini humo wamekamatwa katika maeneo matatu ambayo yana sheria na utawala tofauti ambayo ni Jamhuri ya watu wa China (PRC),Hongkong na Macao na takwimu zinaonesha wafungwa 264 waliwahi kufungwa kuanzia mwaka 2005 na wengi wao wakifanya biashara ya mihadarati.

  Kati ya wafungwa 110 walifungwa China PRC ,80 kifungo cha maisha na wanawake wakiwa 35 katika yao 89 wakiwa kwa kuingiza dawa za kulevya nchini humo na wengine makosa mbalimbali.

  Anasema kati ya wafungwa hao 95 bado wanaendelea na vifungo vyao kwa makosa mbalimbali huku 15 wakitoka.

  Anaeleza kuwa huko Hongkong kwa kipindi hicho walikamatwa watanzania 139 kati yao 135 kwa kuingiza dawa za kulevya, huku wanawake wakiwa 35 na wanne wakifungwa kwa wizi mpaka sasa wamebaki wafungwa 114 na waliotoka ni 20.

  Anasema Macao walikuwa 15 wote walikamatwa kwa kuingiza mihadarati ,wanawake wakiwa watatu na saba tu ndiyo wametoka na kubaki nane.

  Balozi anasema hakuna Mtanzania aliyewahi kunyongwa nchini humo au kuhukumiwa kunyongwa bali wengi wanahukumiwa vifungo vya maisha au vifungo vya miaka mitano hadi 25.

  Anasema hatua hiyo inatokana na kuwa hukumu ya kunyongwa kwa watuhumiwa wa biashara ya mihadarati ni Jamhuri ya watu wa China pekee na siyo kwa Hongkong na Macao.

  Anaeleza bayana kuwa watanzania wengi wameepuka adhabu ya kunyongwa katika utawala wa huo wa China kutokana na kuwepo kwa sheria ambayo mtuhumiwa akikaa miaka miwili baada ya kuhukumiwa kunyongwa na utekelezaji haujafanyika kifungo hicho inakuwa cha maisha.

  Lakini pia ,kutokana na Sheria ya 'Parole' kila mwaka wanaangalia tabia ya mfungwa tangu alipoingia jela na kupewa vigezo vinavyoangaliwa na mfungwa hupewa alama na zikifika kiasi fulani anapunguziwa kifungo cha maisha na kuwa miaka kadhaa"anasema.

  Anasema sheria hiyo pia inawahusu wale waliofungwa miaka kadhaa hivyo si jambo la ajabu nchini humo mtu aliyefungwa maisha akawa huru.

  Anasema kuwa wafungwa nchini China wanalipwa kila mwezi kati ya Yuan 200 hadi 300 ikitegemea uzalishaji aliofanya mfungwa kwa kuangalia asilimia kutokana na kazi za uzalishaji mali kama kushona nguo,viatu na kutengeneza vitu mbalimbali .

  mwisho

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako