• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utekelezaji wa Ukanda Mmoja na Njia Moja wapata msukumo mpya

  (GMT+08:00) 2018-03-05 08:50:18

  na Majaliwa Christopher

  UTEKELEZAJI wa mradi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja umepata msukumo mpya baada ya kutajwa kuwa ni moja ya mambo yanayopewa kipaumbele na Baraza la Mashauriano la Kisiasa la China.

  Hayo yamebainishwa na Mwenyakiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la awamu ya 12, Bw Yu Zhengsheng, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa baraza la 13 wa Mashauriano ya Kisiasa la China.

  Amesisisitiza kuwa baraza hilo, pamoja na mambo mengine, litahakikisisha utekelezaji wa mradi huo kwa ajili ya faida ya mataifa yote husika.

  Mradi wa Ukanda Mmoja Njia Moja, uliyozinduliwa na serikali ya China mwaka 2013 unatarjiwa kugharimu mabilioni ya dola za Kimarekani na utakuwa na faida kwa nchi nyingi za bara la Afrika ikiwemo, Tanzania, Kenya, Djibouti, Ethiopia na Misri.

  Utajumuisha pia mataifa mengine zaidi ya 60 kutoka bara la Asia na Ulaya.

  Itakumbukwa kuwa mwaka jana mwezi wa tano, Serikali ya China ilialika Tanzania kutoka Afrika ya Mashariki kushiriki jukwaa maalum juu ya mradi huu.

  China, nchi ya pili yenye uchumi mkubwa duniani inasemekana tayari imeshafanya uwekezaji kwenye ukanda huo unaogharimu dola za Kimarekani takribani bilioni 60. Inategemewa kuwa uwekezaji huo kwa miaka mingine mitano ijayo utaongezeka na kufikia kati ya bilioni 600 na 800.

  Akitoa ripoti ya kazi kwa niaba ya kamati ya kudumu ya baraza hilo, Bw. Yu amesema wamefanya kazi kubwa katika nyaja mbalimbali za kidiplomasia na kufanya mazungumzo juu ya masuala muhimu yanahusu maendeleo ya China na dunia kwa ujumla.

  Mradi utakapokamilika, utakuwa na faida za kiuchumi kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwani umejikita katika uendelezaji wa miundombinu ambayo ni sekta muhimu katika biashara

  Katika hatua nyingi, Bwana Yu amesema kamati ya Baraza hilo pia imefanya tafiti na mashauriano mbalimbali kuhusu namna bora ya kuendeleza mahusiano yake na nchi zingine duniani ikiwemo pia kuboresha msaada wa sekta ya afya katika bara la Afrika.

  Mkutano huu uliofunguliwa hapo jana (Jumamosi) ulihudhuriwa na rais Xi Jinping na viongozi wengine wa chama na serikali.

  Baraza la 13 la Mashauriano ya Kisiasa lina wajumbe 2,158, ambao nusu kati yao ni wajumbe wapya. Na kiasi cha wajumbe kutoka chama cha kikomunisti cha China ni asilimia 39.8 tu.

  Mwisho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako