• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashindano ya uchoraji ya "Mimi na China"

  (GMT+08:00) 2018-06-29 13:25:18

  Ili kuitikia Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba hapa Beijing, na kuhimiza mawasiliano kati ya Idhaa ya Kiswahili ya CRI na wasikilizaji wetu, Idhaa yetu kwa kushirikiana na mashirika ya China barani Afrika, itazindua mashindano ya uchoraji yaitwayo "Mimi na China" kupitia tovuti yetu ya CRI na kwenye ukurasa wetu wa Facebook.

  Mashindano hayo yanayowalenga wasikilizaji wetu wa Afrika Mashariki, yanakaribisha michoro inayoonyesha jinsi unavyoiona China, au kueleza uelewa wako kuhusiana na China, ambayo inaweza kuakisi urafiki, mawasiliano na ushirikiano kati ya watu wa China na Afrika.

  Ukitaka kushiriki kwenye mashindano hayo, tafadhali tutumie michoro yako ya kidijitali kwenye e-mail yetu: Kiswahili@cri.com.cn, pamoja na maelezo mafupi kuhusu michoro yako, kuanzia Juni 29 hadi Julai 31.

  Matakwa ya michoro yako ni yafuatayo:

  1. Michoro iwe inahusu China;

  2. Michoro iwe ni uliyoichora mwenyewe;

  3. Michoro iwe ya kidijitali, unaweza kuipiga picha kwa simu ya mkononi au kamera, au kui-scan. (Format ya picha iwe JPG, ukubwa wake usipungue 2,000 pixels, na ubora wa picha usipungue 200 dpi.)

  Picha za michoro zitaoneshwa kwenye tovuti yetu ya Kiswahili ya CRI na ukurasa wetu wa Facebook. Kuanzia tarehe 1 hadi 20 mwezi wa Agosti, wasikilizaji wetu wanaweza kupiga kura kwenye mtandao, na wataalamu wa michoro pia watapitia michoro hiyo, na kwa pamoja mtachagua michoro bora. Washindi watapewa tuzo za ngazi tatu zifuatazo.

  1. Tuzo ya Kwanza-Washindi 12 watazawadiwa Simu ya mkononi ya Huawei;

  2. Tuzo ya Pili-Washindi 20, watazawadiwa Simu ya mkononi ya Huawei;

  3. Tuzo ya Tatu –Washiriki 60, watazawadiwa Huawei MediaPad.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako