• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sarakasi yaeneza urafiki

  (GMT+08:00) 2018-08-06 09:40:46

  Liu Yuanpei

  Nikiwa mkalimani, nilikwenda Khartoum, mji mkuu wa Sudan kwa ndege pamoja na kikundi cha ujumbe wa sarakasi kutoka Wuhan, na wanafunzi wa sarakasi wa Sudan.

  Wakati ndege yetu ilipofika uwanja wa ndege wa Khartoum, watu wengi walikuwepo kutukaribisha. Wakuu wa serikali ya Sudan walikuja upande wa kocha wa China, na kupeana mikono na wanafunzi wote. Watu wengi walipiga kelele kwa pamoja "Wachina wa kushangaza" ,"Urafiki kati ya Sudan na China udumu daima"

  Mwaka 1971, miaka 7 baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa China Bw. Zhou Enlai na naibu waziri mkuu Bw. Chen Yi kufanya ziara nchini Sudan, kutokana na makubaliano ya ushirikiano wa utamaduni yaliyosainiwa na serkali za China na Sudan, timu ya wacheza sarakasi kutoka Wuhan ulipokea majukumu ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa sarakasi wa Sudan. Wizara ya utamaduni na elimu ya Sudan ilichagua watoto 50 wenye umri wa miaka 9 kutoka shule mbalimbali nchini humo, na kuwapeleka nchini China kujifunza sarakasi na muziki wa jadi wa China.

  Baada ya mafunzo ya miaka miwili na nusu, watoto hao waliweza kucheza zaidi ya aina 20 za sarakasi. Tarehe 12 mwezi Aprili mwaka 1974, walishiriki kwenye maonesho ya kucheza sarakasi huko Beijing. Maonesho hayo yalifanikiwa na kusifiwa na watu wengi. Chini ya ufuatiliaji wa waziri mkuu Bw. Zhou Enlai na kuungwa mkono na timu ya sarakasi kutoka Wuhan, siku hiyo timu ya sarakasi ya Sudan ilianzishwa rasmi huko Beijing, na watoto hao 50 waliweka msingi wa jukumu la sanaa ya sarakasi nchini Sudan.

  Mwanzoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita, umri wa wanafunzi wa kundi la kwanza ulizidi miaka 20. Walikumbuka sana maisha yao nchini China, na kumkumbuka sana kocha wao waliowafundisha sarakasi. Wakati wa mapumziko, wanafunzi hao wa timu ya sarakasi kutoka Sudan walimzungumka kocha wa China, wakizungumza na kocha huyo kwa lugha ya Kichina, kumuuliza mabadiliko ya China na hali ya walimu wao, kukumbuka maisha nchini China na siku za utoto wao mjini Wuhan.

  Katika muda wa mwaka mmoja na nusu ambapo kocha wa China walitoa mafunzo nchini Sudan, wachezaji wengi wakubwa walifunga ndoa. Tulialikwa kushiriki kwenye sherehe za ndoa zao mara nyingi, hata kocha mmoja alikuwa msimamizi wa ndoa.

  Baadhi ya wanafunzi wakubwa walisema, baada ya kufunga ndoa, wanapanga kutalii nchini China, ambapo watawatembelea walimu wao wa zamani, na kutembelea kwa mara nyingine Ukuta Mkuu, Guilin na Wuhan.

  Tarehe 12 mwezi Aprili mwaka 1981, wakati wa mwaka was saba tangu timu ya sarakasi ya Sudan ilipoanzishwa, wizara ya utamaduni na habari ya Sudan iliandaa hafla ya kutoa nishani kwa kocha wa China.

  Aliyekuwa Rais wa Sudan Gaafar Mohamed Nimeri na mke wake pamoja na balozi wa China nchini Sudan wakati huo Bw.Song Hanyi waliangalia michezo ya sarakasi ya wanafunzi wakubwa na watoto wa timu ya sarakasi ya Sudan.

  Wakati mchezo ulipofikia katikati, sherehe ya kutoa nishani ilianza, rais Nimeri alitoa nishani kwa makocha sita kutoka China. Rais Nimeri alishika mkono wangu akasema "Hongera" kwa lugha ya Kiarabu, mimi nilijibu "Nakushukuru" kwa lugha ya Kiarabu pia. Rafiki wa Sudan wakiwemo maofisa wa Sudan, wakurugenzi wa timu ya sarakasi ya Sudan, na wajumbe wote walipanda jukwaani na kushikana mikono nasi. Kutokana na mpango wa awali, rais Nimeiri alitakiwa kuangalia nusu ya mchezo, kwa kuwa alikuwa na shughuli nyingi, lakini baada ya kutoa nishani aliendelea kuangalia michezo hadi mwisho.

  Kuanzia mwaka 1974 hadi mwaka 2018, timu ya sarakasi kutoka Sudan imepita karibu nusu karne. Mwanzoni kwa kuwa haikuwa na wachezaji, China ilichagua wanafunzi na kuwapatia mafunzo nchini China. Haikuwa na nguo wala vifaa, China ilitoa msaada. Haikuwa na ufadhili wa kutosha wa michezo ya sarakasi, China ilituma walimu hodari zaidi nchini Sudan kutoa mafunzo. Kwa juhudi zake yenyewe, timu ya sarakasi kutoka Sudan ilisifiwa barani Asia na Afrika.

  Wakati tulipotembelea mtaani mjini Khoutoum, baada ya kujua sisi ni makocha wa sarakasi kutoka China, Wasudan walikuwa wanashika mikono yetu, na kutuomba tuwalete watoto wao nchini China kujifunza sarakasi. Hata vijana waliwauliza makocha, "Je, naweza kujifunza sarakasi? Tafadhali nifundishe."

  Sifa ya timu ya sarakasi ya Sudan inaongezeka siku hadi siku, kiwango chake cha sanaa ya sarakasi, na idadi ya wachezaji vyote viko nafasi za mbele katika nchi za kiarabu na kanda ya Afrika Kaskazini. Katika muda mrefu uliopita, timu hiyo ilicheza sarakasi nchini Uganda, Kenya, Kuwait na UAE, na ilipongezwa na kusifiwa sana.

  Nimeondoka nchini Sudan karibu miaka 50, lakini bado nakumbuka mara kwa mara siku zangu nchini Sudan. Nakumbuka sana ndugu wangu wa Sudan. Nina matumaini kuwa urafiki wa sarakasi kati ya China na Sudan utaendelea daima.

  Rafiki mkubwa wa Sudan anayeishi nchini China kwa muda mrefu aliniambia, sanaa ya sarakasi ya China inajenga upya Njia Mpya ya Hariri kutoka China hadi Sudan hata Afrika na dunia ya kiarabu.

   

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako