• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uokoaji wa Wanyamapori

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:41:15

    na Bai Jie

    Nairobi ilikuwa kituo changu cha kwanza cha kazi barani Afrika. Mandhari safi ya kimaumbile, ndege wenye rangi mbalimbali na tumbili wanaoiba matunda kwenye soko la matunda na mbogo pamoja na majengo marefu yalinipa kumbukumbu nyingi. Mchanganyiko wa mambo ya kisasa na mazingira ya kimaumbile ilikuwa chanzo cha mimi kuupenda mji huo.

    Mbali na Nairobi, Masai Mara ni sehemu inayofahamika sana nchini China baada ya sisi kufanya matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni kuhusu uhamaji wa wanyamapori. Mahojiano kuhusu hifadhi ya wanyamapori niliyofanya kwa mara ya kwanza yamenipa uzoefu usiosahauliwa.

    Kuanzia Agosti 10 mwaka 2012, Shirika la WildAid lilianza kufanya matangazo juu ya uwindaji haramu wa wanyamapori likishirikiana na aliyekuwa mchezaji maarufu wa NBA wa China, Bw. Yao Ming. Chaneli ya documentary ya televisheni ya China CCTV, channeli ya Animal Planet na kampuni ya NHNZ ya New Zealand zilishirikiana kutengeneza filamu ya documentary kuhusu hifadhi ya wanyamapori. Nilitumwa kufuatana nao na kuripoti utengenezaji huo.

    Miaka ya sabini na themanini ya karne iliyopita, biashara ya pembe za Ndovu ilishamiri, Tembo wengi wa Afrika waliwindwa, ambao idadi yao ilishuka kutoka milioni 1.3 hadi laki 6. Kufuatia utekelezaji wa mkubaliano ya kupiga marufuku biashara ya pembe za Ndovu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1989, mwelekeo huo ulizuiwa kwa muda. Lakini kutokana na bei ya pembe hizo kupanda siku hadi siku, wawindaji haramu walianza tena kuwawinda Tembo.

    Idara ya usimamizi wa wanyamapori ya Kenya ilitilia maanani katika ziara ya Yao Ming, na kupendekeza mambo mengi kuhusu utengenezaji wa filamu, ili kutangaza umuhimu wa kuhifadhi wanyamapori kwa kupitia umaarufu wa Yao katika jumuiya ya kimataifa na kuimarisha ushirikiano na China katika sekta hiyo. Katika kipindi cha utengenezaji wa filamu, Bw. Yao alitembelea sehemu tano ambako uwindaji haramu wa Tembo ulifanywa. Agosti 16 asubuhi nilifutana na timu yao kutembelea sehemu mbili za mwisho za uwindaji haramu katika mbuga ya wanyama ya Samburu.

    Baada ya kufika katika hifadhi ya Samburu kwa ndege, tulienda sehemu ya kwanza ambako uwindaji haramu ulifanywa. Askari wenye silaha walikuwa kwenye tahadhari kutokana na kugundua nyayo za wawindaji haramu. Tulisikia harufu mbaya tukiwa umbali wa mita kama kumi hivi kutoka mzoga Tembo. Wafanyakazi wa mbuga hiyo walisema, Tembo huyo bado ni mdogo ambaye alifariki ndani ya wiki moja. Wawindaji haramu walikata sehemu kubwa ya kichwa cha Tembo huyo pamoja na pembe zake kabla ya hajafariki, ili waweze kuondoka mapema kukwepa msako wa askari.

    Tembo ni mnyama mwenye upendo na hisia nyingi, na wana akili na busara. Kama Tembo mmoja wa kike akiuawa, mtoto wake atapoteza hamu ya kuishi kutokana na kupotea kwa mama yake. Watoto wengi wa Tembo ambao mama zao wameuawa wanaishi kwenye nyumba ya Tembo yatima iliyoko karibu na bustani ya taifa ya Nairobi. Bw. Yao aliwahi kucheza na Tembo mtoto mmoja. Mwaka 2013, ili kuendelea kutengeneza filamu ya hiyo, Bw. Yao alienda tena nchini Kenya na kumtembelea Tembo mtoto yule, lakini bahati mbaya Tembo yule alifariki kutokana na huzuni ya kumpoteza mama yake.

    Nilitokwa na machozi kutokana na kuona hali halisi ambayo ni tofauti na picha zilizooneshwa kwenye televisheni. Bw. Yao aliniambia kuwa anaweza kunielewa, kwa sababu alishindwa kuzuia huzuni yake na hasira moyoni alipoona kwa mara ya kwanza Tembo waliouawa na wawindaji haramu. Hii imekuwa kumbukumbu ambayo sitaki kukumbuka, ninaweza kukumbuka picha hiyo baada ya miaka kadhaa ninapoangalia filamu za documentary kuhusu Tembo.

    Lakini huzuni siyo utatuzi wa suala, machozi ya watu hayataleta huruma kwa wawindaji haramu. Ninachoweza kufanya ni kuweka kumbukumbu kupitia kamera, na kutumia nguvu yangu kuwafahamisha watazamaji hali halisi ilivyo nyuma ya bidhaa za pembe za Ndovu. Hakuna biashara, hakuna mauaji. Faida kubwa ya pembe za Ndovu na mahitaji ya soko yamesababisha moja kwa moja biashara haramu ya pembe hizo.

    Baada ya kumaliza safari hiyo, niliagana na timu hiyo ya uokoaji wa wanyamapori, Bw. Yao aliendelea na safari yake. Baada ya hapo, watu wengi mashuhuru walianza kujiunga na hifadhi ya wanyamapori kwa njia mbalimbali.

    Wakati rais Xi Jinping wa China akifanya ziara nchini Marekani mwezi Septemba, mwaka 2015, China na Marekani zilifikia makubaliano kuhusu mapambano dhidi ya biashara haramu ya wanyama na mimea ya porini, ambayo ni pamoja na nchi hizo mbili kuahidi kupiga marufuku mauzo na uagizaji wa pembe za Ndovu. Mwishoni mwa mwaka 2016, baraza la serikali ya China lilitoa taarifa ikisema, China itasimamisha shughuli zote za utengenezaji na mauzo ya kibiashara ya pembe za Ndovu na bidhaa zake hadi kufikia Desemba 31 mwaka jana. Inamaanisha kuwa, kuanzia siku hiyo, marufuku ya biashara ya pembe za Ndovu inatimizwa kwa pande zote nchini China. Hatua hiyo imeonesha hadhi ya nchi kubwa ya China inayotekeleza wajibu wake, ambayo inapongezwa na walinzi wa mazingira kote duniani.

    Katika matangazo mapya ya hifadhi ya wanyamapori ya mwaka huu, Bw. Yao amesema, bei ya bidhaa za pembe za Ndovu ni ghali sana, gharama kubwa haitokani na bei yake, bali inatokana na thamani ya maisha ya Tembo. Nchi yetu imetekeleza sera ya kupiga marufuku biashara ya pembe za Ndovu, sheria imezifanya pembe hizo kutokuwa bidhaa tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako