• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uzoefu wangu Malawi ulikuwa kama mafunzo ya kiroho

  (GMT+08:00) 2018-08-06 09:41:46

  Ili kutimiza ndoto yangu na kufika mbali zaidi, niliondoka nyumbani na na kuagana na wazazi na marafiki zangu, na kufunga safari tena ya kwenda mbali ambako sijawahi kufika. Kama nikisema kuchagua kwenda Afrika ni kuiga mifano ya Meryl Streep na Audrey Hepburn, basi kuichagua Malawi ni kama hatma yangu, ambako nitaona mandhari nilizoandikiwa kuziona, na kukutana na watu nilioandikiwa kuwakuta.

  Kabla ya kuja Malawi, nilikuwa mtu wa kupenda sana kulala, lakini baada ya kuja hapa nimebadilika. Kila asubuhi naamshwa na mwanga wa jua na sauti za ndege. Hapa Malawi hakuna majira ya baridi, kila majira maua yenye rangi tofauti yanachanua, hii ni hali inayofurahisha sana macho. Lakini licha ya mambo hayo mazuri, pia kuna mabaya. Moja ni kukatika kwa umeme mara kwa mara, haswa usiku. Katika giza totoro, sauti yoyote, ya wadudu, ya mbwa, na hata ya maua, inasikika vizuri. Nchini Malawi hatari huambatana na giza. Wakati wa usiku, hata wenyeji hawathubutu kutoka nje ovyo, kwa hivyo sikuwahi kutoka nje hata mara moja baada ya usiku kuingia.

  Mbali na mandhari nzuri zilizofurahisha macho yangu, pia kulikuwa na mambo mengi yaliyogusa moyo wangu, haswa wakati nilipokuwa shuleni. Niliguswa sana wakati nilipoona mara ya kwanza maneno ya Kichina kama vile "China", "Ndoto ya China" na "Nataka kwenda China", yaliyoandikwa kwenye mabegi ya wanafunzi wa Zambia; Niliguswa sana wakati nilipopokea zawadi ya "tambi za haraka" kutoka kwa mtoto mmoja, ambayo kwake anadhani ni "kitoweo adimu"; Pia niliguswa sana wakati nilipokumbatiwa na wanafunzi watoto na kuambiwa kwamba wamenikumbuka sana…Watoto hao wa Zambia wamevuka sana matarajio yangu, na ni wao walionifanya nielewe maana na umuhimu wa kuja kufanya kazi hapa.

  Nchini Malawi watoto wenye miaka sita au saba tu wameanza kuchukua wajibu wa kuwaangalia wadogo wao, ili kuwasaidia wazazi kutunza familia. Siku moja niliona wavulana wenye miaka nane au tisa wakiwa wamejitwishwa kuni nyingi kichwani, wakati waliposimama na kupumzika, niliwakaribia na kujaribu kuwatua kuni kutoka kichwani, lakini ilikuwa ni "aibu kidogo" kwamba hata nilishindwa kufanya hivyo, watoto hao walipoona hivyo, wakaonesha tabasamu. Huenda kwao jambo lilikuwa la kuchekesha, lakini nilijisikia maumivu moyoni. Ili kuwatafutia chakula wadogo wao, mara kwa mara walikuwa wanaondoka nyumbani saa tatu usiku, kwenda maeneo ya mbali sana mlimani kuokota kuni, na asubuhi ya siku ya pili watasafirisha nje kuni walizookota kwa kuzibeba kichwani. Waliniambia kuwa safari hiyo ya kawaida huchukua saa 12, na kipato wanachopata hakitoshi kununua mlo mmoja wa mchana kwenye mgahawa. Jambo baya zaidi ni kwamba hawakuwa na viatu, siwezi kufikiria jinsi walivyoweza kuvumilia miba, nyoka na wadudu walipotembea kwa miguu msituni. Niliwahi kufikiria kuishi kama wao kwa siku moja tu, lakini mpaka sasa sijapata ujasiri wa kufanya hivyo, hata sijathubutu kutembea nje kwa miguu bila viatu. Maisha nchini Malawi kweli ni magumu, lakini yanaweza kuwa rahisi kidogo ukiwa na matarajio na matumaini moyoni.

  Uzoefu wangu nchini Malawi ni kama mafunzo ya kiroho. Tangu Siku ya kwanza nilipokanyaga ardhi ya nchi hiyo, niliichukulia kila siku niliyofanya kazi nchini humo kama zawadi kwa maisha yangu. Niliyoona na nilivyojisikia hapa vimenifanya nithamini maisha, na kuishi kwa makini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako