• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CRI Nairobi 91.9 FM -- Tangazo la Nafasi za Kazi

    (GMT+08:00) 2019-03-18 09:19:29

    CMG Kiswahili inawakaribisha wakenya wenye uwezo wa kutoa ripoti, kutangaza, kuhariri, kutengeneza video na mambo ya masoko, watoe maombi ya nafasi za kazi kwenye kituo chetu cha Nairobi, ili tuimarishe pamoja matangazo yetu kwa wasikilizaji, wasomaji na watazamaji wetu.

    CMG Kiswahili ni sehemu moja ya Kituo Kikuu cha Radio na Televisen cha Taifa cha China kinachounganisha China Global Television Network, Radio ya Serikali kuu ya China (CNR) na Radio China Kimataifa (CRI). Lengo letu ni kuitangaza China barani Afrika, na kulitangaza bara la Afrika nchini China, kutangaza mambo ya dunia barani Afrika, na kuongeza maelewano na urafiki kati ya watu wa China na wa Afrika. Wenye sifa kama zifuatazo wanakaribishwa kututumia maombi:

    A. Watangazaji, Wahariri na Waandishi wa habari : ( Nafasi saba )

    * Masharti ya kimsingi kwa mwombaji:

    1. Awe na elimu isiyopungua Shahada ya kwanza

    2. Awe na umri wa chini ya miaka 40

    * Sifa ya Mwombaji

    1. Awe na uwezo mzuri wa kukusanya, kuandika na kutangaza habari kwa lugha ya Kiswahili. Awe na uzoefu wa kazi katika vyombo vya habari (anayefahamu lugha ya Kichina atapewa kipaumbele).

    2. Awe mfuatiliaji wa mambo ya habari, habari kuhusu China na wimbi la kisasa (Mwenye ujuzi kuhusu mambo ya Internet na New Media atapewa kipaumbele).

    3. Awe na uwezo wa kushirikiana na wenzake, anayependa kujifunza, kukabiliana na shinikizo, kupokea na kuzoea kwa haraka mawazo mapya, ujuzi mpya na teknolojia mpya.

    4. Awe na afya nzuri, anayeweza kuvumilia kazi katika muda usio wa kawaida: kwa mfano kuanza kazi saa 12:00 asubuhi au kumaliza kazi saa 4:00 usiku; na kuweza kufanya kazi kwa muda wa ziada , na kusafiri kikazi.

    * Majukumu:

    1. Kukusanya, kuhariri na kutangaza habari kwa lugha ya Kiswahili, kwa ajili ya mahitaji tofauti ya Radio, Facebook, Tovuti, na APP.

    2. Kutoa ripoti na kuandika habari kwa Kiswahili na kupiga picha za matukio na masuala yanayofuatiliwa kwenye jamii.

    3. Kushiriki/kuchangia kwenye matangazo ya Kiswahili ya moja kwa moja (habari, maelezo na muziki).

    * Kituo cha kazi : Nairobi

    * Zamu za kazi: Asubuhi na jioni, na Zamu za wikiendi zinabadilika kila baada ya muda.

    * Wakati unaotarajiwa kuanza kazi : Mwezi Julai, 2019

    * Mwombaji anatakiwa kututumia CV kupitia E-Mail: kiswahili@cri.com.cn kabla ya Aprili 30, 2019 iwe na kichwa cha "Jina + Mtangazaji, Mhariri na Mwandishi wa habari wa Kiswahili".

    B. Watangazaji wa Radio ya Kiswahili ( nafasi saba )

    * Masharti ya kimsingi kwa mwombaji:

    1. Awe na Elimu isiyopungua Shahada ya kwanza

    2. Awe na umri wa chini ya miaka 40

    * Sifa ya Mwombaji

    1. Awe na uwezo mzuri wa kukusanya, kuandika na kutangaza habari kwa lugha ya Kiswahili. Awe na uzoefu wa kazi katika vyombo vya habari (anayefahamu lugha ya Kichina atapewa kipaumbele).

    2. Awe mfuatiliaji wa mambo ya habari, habari kuhusu China na wimbi la kisasa, awe na uwezo wa kuendesha vipindi vya mijadala na vipindi vya muziki, anayeuelewa muziki, na awe na ujuzi kuhusu utamaduni wa kwenda na wakati. Awe na ujuzi wa kutumia software mbalimbali za kuchanganya sauti, awe na ujuzi kuhusu teknolojia za mtandao wa Internet, na New Media.

    3. Awe na uwezo wa kushirikiana na wenzake, kupenda kujifunza, kukabiliana na shinikizo bila hofu, anayeweza kupokea na kuzoea mawazo mapya, ujuzi mpya na teknolojia mpya.

    4. Awe na afya nzuri, na awe mtu wa kuweza kuvumilia kazi katika muda usio wa kawaida: kwa mfano kuanza kazi 12:00 asubuhi au kumaliza kazi saa 4:00 usiku, na kuweza kuvumilia kufanya kazi kwa muda wa ziada au kusafiri kikazi.

    * Majukumu:

    1. Kushiriki kwenye matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya Kiswahili ( habari, maelezo, mijadala na muziki)

    2. Kushughulikia ujenzi na utunzaji wa maktaba ya muziki ya kidijitali

    * Kituo cha kazi : Nairobi

    * Wakati unaotarajiwa kuanza kazi: Mwezi Julai mwaka 2019

    * Mwombaji anatakiwa kututumia CV kupitia barua pepe (E-Mail): kiswahili@cri.com.cn, iwe na kichwa cha "Jina + Mtangazaji wa Radio wa Kiswahili"

    C. Waandishi wa habari wa vyombo vipya vya habari(New Media) ( Nafasi tano )

    * Masharti ya kimsingi:

    1. Awe na Elimu isiyopungua Shahada ya kwanza

    2. Awe na umri wa chini ya miaka 35

    * Sifa ya muombaji :

    1. Awe na uwezo mzuri katika kukusanya, kuhariri au kutangaza habari kwa Kiswahili. Awe na uzoefu wa kazi katika vyombo vya habari, na anayefahamu lugha ya Kichina atapewa kipaumbele.

    2. Awe mfuatiliaji wa wimbi la kisasa kwenye vyombo vipya vya habari hususan mitandao ya kijamii, awe na uwezo wa kutambua matukio ya dharura na yanayofuatiliwa kwenye mtandao wa Internet, na kuwa na uwezo wa kupiga video na kuzitengeneza, na awe na uwezo wa kuwa mtangazaji wa video.

    3. Anayependa kufanya kazi kwa hiari na mbunifu, awe na moyo wa kushirikiana na wenzake katika timu ya kazi, anayependa kujifunza, anayeweza kukabiliana na shinikizo bila hofu, anayeweza kupokea na kuzoea mawazo mapya, ujuzi mpya na teknolojia mpya.

    4. Awe na afya nzuri, anayeweza kuvumilia kazi katika muda usio wa kawaida, kwa mfano: Kuanza kazi 12:00 asubuhi au kumaliza kazi saa 4:00 usiku, na kuweza kufanya kazi kwa muda wa ziada na kusafiri kikazi

    * Majukumu:

    1. Kushirikiana na timu ya kazi katika kuandaa, kupiga picha na kutengeneza video fupi kwenye vyombo vipya vya habari.

    2. Kuchagua mada za vipindi, kufanya shughuli za matangazo kwenye mtandao wa Internet au nje ya mtandao wa Internet.

    * Kituo cha Kazi: Nairobi

    * Wakati unaotarajiwa kuanza kazi: Mwezi Julai, 2019

    * Mwombaji anatakiwa kututumia CV kwa barua pepe (E-mail) Kiswahili@cri.com.cn, iwe na kichwa cha "Jina la Mhariri+mwandishi wa habari wa Kiswahili".

    D. Msimamizi Mkuu wa uendeshaji wa shughuli zinazohusu lugha ya Kiswahili ( Nafasi moja )

    * Masharti ya kimsingi kwa mwombaji:

    1. Awe na Elimu isiyopungua Shahada ya kwanza

    2. Awe na umri wa chini ya miaka 40

    * Sifa ya mwombaji:

    1. Awe na uzoefu wa kazi katika uendeshaji wa shughuli za vyombo vya habari, raslimali nzuri ya watu wa sekta mbalimbali.

    2. Anayebeba wajibu kwa makini, awe na uwezo mzuri wa kufanya uratibu na mawasiliano na watu, na kudumisha uhusiano mzuri na washirika na wateja.

    3. Awe na uwezo wa kufanya utafiti wa masoko, kuunganisha raslimali, kufanya usimamizi wa vyombo vya habari, na kuanzisha soko.

    4. Awe na afya nzuri, anayeweza kuvumilia kazi katika muda usio wa kawaida, na kuweza kuvumilia kazi kwa muda wa ziada na kusafiri kikazi

    * Majukumu:

    1. Kushughulikia matangazo ya shughuli mbalimbali za CMG Kiswahili, kushiriki kwenye shughuli za mtandao wa Internet na nje ya mtandao wa Internet, huku akiwa na kazi nyingine za Studioni.

    2. Kuwasaidia wafanyakazi wenzake kufanya uhariri na kazi nyingine.

    * Kituo cha kazi : Nairobi

    * Wakati unaotarajiwa kuanza kazi: Mwezi Juni mwaka 2019

    * Mwombaji anatakiwa kututumia CV kwenye barua pepe (E-Mail): kiswahili@cri.com.cn, iwe na kichwa cha "Jina + Msimamizi Mkuu wa Uendeshaji wa shughuli".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako