• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania kujifunza katika jimbo la Hebei China kutangaza rasilimali zilizopo kuvutia watalii

  (GMT+08:00) 2019-05-07 13:04:03

  Theopista Nsanzugwanko,DAR ES SALAAM

  TANZANIA na Jimbo la Hebei lililopo nchini China wamekutana kubadilishana uzoefu kuhusu namna ya kuongeza idadi ya watalii wa pande hizo mbili .

  imeelezwa kuwa jimbo la linapokea watalii milioni moja kwa mwaka kutokana na kutangaza vema vivutio vyake ikiwa ni pamoja na kuanzisha utaratibu wa kutembelea nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuhamasisha utalii wa mji huo.

  Mkurugenzi wa Kituo cha China Gao Wei anasema hayo baada ya wajumbe wa jimbo hilo la Hebei kufika nchini Tanzania na kukutana na baadhi ya watumishi kutoka Bodi ya Utalii Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kuhusu utalii wa nchi hizo mbili.

  Katika jimbo hilo kuna vivutio mbalimbali vikiwemo vya barafu na theluji, chemchemi ya maji ya moto pamoja na vivutio vingine ikiwemo maonesho ya tamaduni mbalimbali za China.

  Anasema jimbo hilo lina utajiri wa Maliasili hivyo wamekuwa na mikakati mizuri ya kutangaza utalii uliopo .

  Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Devota Mdachi alisema wamekutana na ujumbe wa utalii kutoka jimbo hilo la China kwa ajili ya kuangalia shughuli wanazoweza kushirikiana nao katika masuala ya utalii.

  Mdachi alisema jimbo la Hebei lililopo China wanapokea watalii milioni moja kwa mwaka huku Tanzania kwa mwaka nchi nzima inapokea watalii milioni 1.5 hivyo kwa maendeleo hayo makubwa jimbo linaonesha jinsi walivyoweka mikakati ya kutumia rasilimali walizonazo.

  Anasema bodi ya utalii nchini imeona jiji la Dar es Salaam pekee linaweza kuwa na utalii wake na kujitangaza kama jimbo hilo lililopo China.

  Anasema Septemba mwaka huu jimbo hilo lina maonyesho nchini kwao hivyo kwa Tanzania hiyo ni fursa kwenda na kujifunza baada ya kujifunza huko nao watawaalika wachina kuja kwenye onyesho la lugha ya Kiswahili linalofanyika Oktoba mwaka huu.

  mwisho

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako