• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahitimu wa vyuo vikuu wakabiliwa na changamoto kutafuta ajira kutokana na janga la COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-07-29 14:00:07


    Mlipuko wa virusi vya Corona ulioibuka ghafla mwanzoni mwaka huu umewafanya wanafunzi wa vyuo vikuu wanaohitimu mwaka huu wakabiliwe na changamoto kubwa ambayo hawakutarajia katika kutafuta ajira.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Elimu ya China, idadi ya wanafunzi watakaohitimu vyuo vikuu mwaka huu itafikia milioni 8.74, likiwa ni ongezeko la wahitimu laki nne kuliko mwaka jana. Ongezeko hilo pamoja na athari za janga la COVID-19, vimetoa changamoto kubwa kwa wahitimu wa mwaka huu kwenye kutafuta ajira.

    Ripoti kuhusu ajira za wahitimu wa vyuo vikuu kwa mwaka huu iliyotolewa kwa pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Ajira ya Chuo Kikuu cha Umma cha China na wakala wa huduma za ajira wa Zhaopin, inaonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu idadi ya nafasi za ajira kwa wahitimu wapya wa vyuo vikuu imepungua, huku idadi ya waombaji wa nafasi za ajira ikiongezeka kwa asilimia 143.25 katika mwezi wa Machi.

    Hali hiyo imewafanya wahitimu wengi wa mwaka huu waahirishe mpango wao wa kutafuta ajira wanazotarajia hadi mwaka kesho, baadhi yao wameamua kutumia muda huu kutembelea sehemu mbalimbali za China, au kujitolea kujiunga kwenye mpango wa taifa wa kuunga mkono ujenzi wa sehemu ya magharibi ya China.

    Ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni na Idara ya takwimu ya taifa kuhusu ajira za wahitimu wa vyuo vikuu mjini Shanghai mwaka huu inaonesha kuwa, asilimia 34 ya wahitimu wamebadilisha mpango wao wa awali wa kutafuta ajira, kati yao asilimia 90.4 wameamua kuendelea na masomo ya shahada ya juu zaidi, huku asilimia 9.6 wakichagua kuahirisha mpango wa kutafuta kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako