• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazazi wa Beijing wakumbwa na changamoto kutokana na madarasa ya watoto kwa njia ya mtandao

    (GMT+08:00) 2020-07-24 20:08:27


    Kutokana na maambukizi mapya ya virusi vya Corona, Beijing ilitangaza kuinua kiwango cha tahadhari ya dharura ya afya ya umma kutoka kwa tatu hadi mbili. Baadaye idara ya Elimu ya Manispaa ya Beijing ilitangaza kwamba kuanzia Juni 17, madarasa yote ya shule za msingi na sekondari yatafanyika nyumbani kwa njia ya mtandao wa Internet. Kabla ya hapo, kwa sababu ya athari ya janga la COVID-19, wanafunzi wa mji wa Beijing walikuwa wanasoma nyumbani kwa zaidi ya miezi mitatu, na walirudi shuleni kwa wiki moja tu. Aidha idara hiyo pia iliwataka wanafunzi wote wawe tayari kurudi kwenye madarasa ya shuleni au kuendelea kusoma nyumbani katika muhula ujao. Wazazi wa Beijing wameshtushwa na habari hizo, na kusema wanakaribia kuchanganyikiwa!

    Lakini kwa wanafunzi wa Beijing, kusoma nyumbani ni kama kusoma shuleni, licha ya masomo mbalimbali, hafla ya kupandisha bendera ya taifa na mazoezi ya kujenga mwili vyote havikosekani. Wazazi wanachukuliwa kama ni nusu walimu. Licha ya kuwafundisha watoto, kwa mujibu wa maagizo ya walimu, wazazi wanatakiwa kupiga picha ya watoto wanaovyosoma nyumbani, na kuzituma kwa walimu pamoja na kazi za watoto baada ya madarasa. Kwa wazazi wanaokaa nyumbani, wanaweza kujaribu kushinda kazi hizo kirahisi, lakini wazazi wengi pia ni wafanyakazi, kwa hiyo hiyo ni kazi ngumu kwao. Hata hivyo baadhi ya wazazi wanaona hii ni fursa nzuri kwao kushiriki kwenye masomo ya watoto wao, na pia ni njia mwafaka ya kuimarisha uhusiano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako