Matukio ya magari ya wagonjwa kuzuiliwa barabarani yatokea mara kwa mara
2020-08-27 11:03:34| CRI

Matukio ya magari ya wagonjwa kuzuiliwa barabarani yatokea mara kwa mara

Uokoaji wa maisha ya watu unapaswa kufanyika kwa wakati, na gari la wagonjwa linapopita barabarani inamaanisha kuwa linashindana na wakati, kwani inahusiana na usalama wa maisha ya watu. La muhimu zaidi ni kuwa, kanuni za usalama wa mawasiliano barabarani pia zimeweka kipaumbele cha matumizi ya barabara kwa ajili ya magari ya wagonjwa. Hata hivyo hali ya kuyakwamisha magari ya wagonjwa inatokea mara kwa mara.

Tarehe 30 mwezi Julai mwaka huu, gari moja la wagonjwa lilizuiliwa na pikipiki moja kwenye njia ya kuelekea hospitali mjini Chaozhou, mkoani Guangdong. Mwendesha pikipiki alikataa kulipisha gari la wagonjwa baada ya kushawishiwa na wapita njia. Baada ya hapo, polisi ya huko ilimtoza mwendesha huyo wa pikipiki faini ya yuan 1,900, sawa na dola za kimarekani 270, na kuadhibiwa kwa kukatwa pointi 3, kutokana na ukiukwaji wa kanuni nyingi za usalama barabarani.

Mwezi Juni mwaka huu, gari moja lililombeba mjamzito aliyetokwa damu kwa wingi mjini Qinzhou, mkoani Guangxi, lilizuiliwa na gari moja dogo barabarani. Kutokana na barabara lkuwa jembamba, baada ya kupiga king'ora tahadhari mara nyingi, gari dogo halikupunguza mwendo au kulifanya gari la wagonjwa lipite, hali ambayo ilichelewesha gari la wagonjwa dakika kadhaa kupita barabara hapo. Wakati mjamzito aliposafirishwa hopitalini alikuwa amekutwa na hali ya hatari. Imefahamika kuwa endapo mjamzito angechelewa kwa dakika kadhaa zaidi, basi maisha yake pamoja na ya mtoto mchanga yangepotea. Mwendesha wa gari dogo alitozwa faini dola za kimarekani 30, na kuadhibiwa kwa kupunguza pointi 3 kwenye rekodi yake ya leseni ya udereva.