Msichana akataa kupanda gari na mfanyakazi wa usambazaji wa vifurushi
2020-08-27 10:39:12| CRI

Msichana akataa kupanda gari na mfanyakazi wa usambazaji wa vifurushi

Hivi karibuni, mwanamke mmoja alikataa kupanda Taxi pamoja na mfanyakazi wa usambazaji wa vifurushi, na kuzusha mjadala kwenye mtandao wa kijamii.

Mmoja wa Abiria aliyepanda Taxi hiyo Xiao Lu alieleza kuwa, wao watatu waliita Taxi hiyo kupitia App ya simu ya mkononi, na yule mwanamke alikuwa mtu wa mwisho aliyefika. Alipofika aligundua kuwa mfanyakazi wa usambazaji wa vifurushi alikuwa amekaa ndani ya Taxi kwa hiyo alikataa kupanda, na kumtaka mfanyakazi wa kusambaza vifurushi ashuke. Dereva alieleza kuwa, abiria wote wana haki sawa, na kama mwanamke huyo hataki kuipanda Taxi yake anaweza kuita taxi nyingine. Lakini mwanamke huyo alishikilia kuwa amelipia gharama hivyo ni lazima apande.

Dereva alisema amewapakia abiria wengi walioita Taxi kwa pamoja wakiwemo mabosi wakubwa, lakini hajawahi kukutana na mtu kama mwanamke huyo anayedharau abiria wengine na kuwarushia maneno mabaya. Hatimaye dereva huyo aliamua kuondoka na abiria wengine wawili.