Msichana nyota mwenye umri wa miaka 8 awa jaji wa mashindano
2020-08-31 21:06:13| CRI

Msichana nyota mwenye umri wa miaka 8 awa jaji wa mashindano


Hivi karibuni yalifanyika mashindano ya kuimba huko mjini Jining, mkoani Shandong nchini China na kusababisha mjadala mkubwa. Sio kwa sababu onesho lilikuwa ni la ajabu, bali majaji wake ni wa kushangaza sana. Mtoto wa miaka minane alikuwa jaji na alitoa maoni juu ya matamshi na beats za washindani. Msichana huyo mdogo hakuogopa hata kidogo.

Maswali ya watazamaji yaliegemea zaidi katika mambo mawili: Kwanza, je! Unafahamu wa mtoto huyo mwenye miaka minane tu juu ya nadharia na ufahamu wa muziki unaweza kumsaidia kutoa maoni yake juu ya nyimbo hizi za watu wazima? La pili ni kwamba, je upande wa kuanzisha maonesho hayo unalenga kuwavutia watazamaji kwa kupitia njia hiyo?

Msichana huyo anayeitwa Xiao Yuyu ni mkazi wa mji wa Jining. Amekuwa nyota tangu alipokuwa na umri wa miaka miwili ambaye alipokuwa mwimbaji mdogo. Aliwahi kushiriki kwenye vipindi vya kituo cha televisheni CCTV, na vipindi vingine mbalimbali vya televisheni. Anajulikana kwa watu wengi zaidi kutokana na fursa hii ya kuwa jaji.

Baba wa Xiao Yuyu alisema wakati alipohojiwa na waandishi wa habari, kuwa jambo hilo limeleta shinikizo kubwa kwa familia yake, hivi sasa hawezi kudokeza mambo mengi zaidi, na kutumai watu wasimdhulu Xiao Yuyu ambaye bado ni mtoto .