Kesi za wanawake waliouawa na waume zazusha mjadala mkubwa
2020-08-31 20:59:51| CRI

Kesi za wanawake waliouawa na waume zazusha mjadala mkubwa


Mwanamke mmoja wa Kusini Magharibi mwa mkoa wa Sichuan aliripotiwa kuuawa na mumewe wakati amelala. Kesi hiyo imezusha mjadala kwenye mtandao wa kijamii kwamba hii ni kesi nyingine ya mume kumuua mke kama iliyotokea kwenye mkoa wa Zhejiang, kesi ambayo ilifuatiliwa na watu kutokana na ukatili wa mume huyo na tabia yake ya utulivu baada ya kufanya mauaji.

Mwanamume Qu mwenye umri wa miaka 30 huko Anyue, Sichuan, alimwua mkewe na kuwaita polisi siku iliyofuata. Hali hii inafanana na kesi ya huko Zhejiang, ambapo muuaji anayeitwa Xu alimwua mkewe asubuhi na kuwaambia polisi siku moja baadaye kwamba "mkewe alikuwa amepotea."

Ingawa mambo halisi kuhusu kesi ya Qu hayajatangazwa, lakini kupitia video ya CCTV, alionekana akichukua koti chini ya ghorofa ya jengo lake na kmhusisha na tukio hilo. Katika kesi ya Zhejiang, Bw Xu alitupa mwili wa mke wake kwenye tanki ya maji taka kwenye makazi yake. Mambo ya kufanana kati ya mauaji hayo mawili yamezusha mjadala kwenye mtandao wa kijamii kuwa ripoti za kesi ya Xu zilimchochea Qu kumwiga muuaji wa kwanza, na kwamba itaweza kusababisha kesi nyingi zaidi za uhalifu wa kuiga. Baadhi ya watu wanaona polisi hawapaswi kutangaza mambo mengi halisi kuhusu mauaji, wanachotakiwa kufanya ni kutangaza uamuzi wao na adhabu zitakazotolewa dhidi ya wauaji, ili kuzuia wengine kuiga.

Ripoti iliyotolewa mwaka 2019 na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mambo ya Dawa za kulevya na Uhalifu kuhusu mauaji ya wanawake imeenea kwenye mtandao wa Internet, ambayo inasema utafiti unaonyesha kwamba idadi kubwa ya waathirika wa kike wa mauaji kote duniani waliuawa na waume au jamaa zao.