Soko la Xinfadi la Beijing lafunguliwa tena
2020-09-09 10:40:15| CRI

Soko la Xinfadi la Beijing lafunguliwa tena

Baada ya kusimamishwa kwa Soko la Xinfadi la Beijing kwa miezi miwili kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, kuanzia tarehe 15 Agosti, eneo la kusini la soko hilo limefunguliwa rasmi, na soko hilo litafunguliwa kabisa kuanzia tarehe 10 Septemba. Baada ya kufunguliwa tena, soko hilo halitafanya biashara ya rejareja, litashughulikia mauzo ya jumla tu, na soko lenye eneo la mita za mraba 1000 litajengwa nje kushughulikia biashara ya rejareja kwa wakazi.

Pande zote mbili za wateja na wauzaji wanahitaji kujiandikisha kwenye soko hilo, na pia wanapaswa kuweka oda ua uagizaji (reservation), kuonesha leseni ya magari, kutaja hali halisi kuhusu sehemu na wakati wa kufanya biashara, na mlango wa kuingia kwa magari, halafu wanaweza kufanya biashara. Mbali na hayo ni magari ya pande mbili za kufanya biashara tu yatakayoruhusiwa kuingia, na watu wote watakaoingia sokoni wanapaswa kupitia utambuzi wa sura na upimaji wa joto la mwili.

Naibu meneja mkuu wa soko la Xinfadi Bw. Gu Zhaoxue ameeleza kuwa, lengo la hatua hizo ni kukusanya taarifa halisi za watu na magari, ili kuongeza ufanisi wa usimamizi wa soko, na kuweka msingi wa kisayansi wa usimamizi wa soko na mahitaji na utoaji wa bidhaa za mazao ya kilimo.