China yapongeza mafanikio yaliyopatikana katika miaka 20 tangu FOCAC kuanzishwa
2020-11-13 19:27:36| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin leo amesema, kutokana na juhudi za pamoja za China na Afrika za miaka 20 iliyopita, baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC limekuwa jukwaa muhimu na utaratibu wenye ufanisi wa kuimarisha mshikamano na urafiki kati ya China na Afrika, kuhimiza maendeleo ya pamoja kati ya China na Afrika na kuhimiza urafiki kati ya watu wa China na Afrika. Mafanikio ya ushirikiano kupitia baraza hilo yananufaisha watu wa China na Afrika.

Bw. Wang amesema katika hafla ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa FOCAC, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ametoa mapendekezo manne kuhusu kuhimiza baraza hilo kuendelea kuongoza maendeleo yenye uvumbuzi ya uhusiano kati ya China na Afrika, kupendekeza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika, jumuiya ya pamoja ya afya na jumuiya ya pamoja ya maendeleo, na kushirikiana katika kujenga jumuiya ya binadamu ya mustakabali wa pamoja .