Umoja wa Ulaya wajadili kuhusu kuongeza uratibu katika kupambana na janga la COVID-19
2020-11-20 18:55:15| cri

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefanya mkutano kwa njia ya video kwa lengo la kujadili mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona, huku mada kuu katika mkutano huo ikiwa ni kuongeza uratibu katika upimaji wa haraka, utoaji wa chanjo na muda wa kuondoa zuio.

Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula von der Leyen amesema, upimaji wa nucleic acid ni njia bora lakini gharama yake ni ya juu na kasi yake ni ndogo. Lakini, upimaji wa Antigen ni rahisi zaidi ambao unaweze kutumiwa katika udhibiti wa kikanda, kufuatilia wagonjwa na upimaji wa kawaida.

Rais wa Baraza la Ulaya Bw. Charles Michel amesema, nchi wanachama wa Umoja huo zinapaswa kufanya maandalizi na kuandaa mpango wa kutoa chanjo, kwa kuwa baadhi ya nchi hazina uwezo wa kuhifadhi na kusafirisha chanjo.