Ethiopia yatarajia kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na China
2020-11-25 19:50:18| CRI

Katika mazungumzo ya 12 ya ushirikiano wa uwekezaji ya China, Balozi wa Ethiopia nchini China ameeleza matarajio yake ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, na kukaribisha China kuwekeza nchini mwao.

Balozi wa Ethiopia nchini China Bw. Teshome Toga Chanaka amesema, China na Ethiopia zimejenga ushirikiano wa karibu katika sekta za kilimo na ujenzi wa miundo mbinu, na kufanya miradi mbalimbali ya ushirikiano. Amesema hata hivyo nchi hizo mbili zinaweza kupanua zaidi ushirikiano.

“tunapaswa kusukuma mbele zaidi hali hii ya sasa. Kabla ya hapo serikali ya Ethiopia ilitoa mpango wa maendeleo ya miaka 10, ambayo yanazingatia uchumi wa kidijitali, TEHAMA, rasilimali watu, utalii na sekta nyingine mpya, vilevile sekta ya usafiri wa anga, hivyo sisi tutakuwa na mawasiliano rahisi kati yetu na China. Kwenye msingi wa ushirikiano ulivyo sasa kati yetu, tunaweza kupanua zaidi wigo wa ushirikiano wetu. ”