Umoja wa Ulaya watangaza mpango mpya wa maingiliano na wahamiaji
2020-11-25 09:01:33| CRI

Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imetangaza mpango mpya wa utendaji ili kuboresha maingiliano na ujumuishaji wa wahamiaji katika Umoja huo. Hatua za mpango huo zitaangalia elimu na mafunzo kwa wahamiaji, fursa za ajira na utambuzi wa ujuzi, upatikanaji wa huduma za afya, na pia nyumba bora na za bei nafuu. Umoja huo umesema, mpango huo utawahimiza wahamiaji kutumia ipasavyo uwezo wao, na pia jumuiya ya Ulaya itanufaika na uwezo na ujuzi wao.