Kilimo ndio kitakacholeta ahueni ya kiuchumi kwa nchi za Afrika ,yasema IMF
2020-11-25 17:01:28| cri

Nchi za Afrika zinazotegemea mno sekta ya utalii zinakabiliwa na kipindi kigumu cha ufufukaji baada ya janga la Covid-19, ambalo linaendelea kusababisha maafa katika uchumi wa mataifa mbalimbali duniani.

Wachumi kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Renaissance Capital wanakadiria kuwa nchi zenye sekta kubwa za kilimo na utegemezi mdogo wa utalii zitafufuka mapema kutokana na makali ya kiuchumi yaliyosababishwa na janga la Covid-19.

Kulingana na IMF,athari kubwa za janga la Covid-19,katika ukuaji wa uchumi,zimepatikana katika nchi zinazotegemea utalii kama vile Mauritius ,ushelisheli, Cabo Verde, Comoros na the Gambia japokuwa nchi zenye kusafirisha bidhaa pia zimeathirika mno.

Kwa nchi zenye kutegemea utalii,sekta hiyo inawakilisha asilimia 18 ya pato la taifa kwa wastani na inachukua jukumu kubwa katika kusaidia maisha ya watu,na pia inachangia asilimia 25 ya jumla ya ajira.

Utalii pia ni chanzo muhimu cha mapato ya fedha,ukichangia asilimia 18 ya mapato nchini Ushelisheli.

Licha ya ahueni ya ulimwengu katika sekta nyingi,mapato ya utalii hayatarajiwi kuerejea katika viwango vya mwaka 2019 hadi mpaka mwaka 2023.