Kituo cha ushirikiano wa uhifadhi wa mazingira kati ya China na Afrika chazinduliwa Beijing
2020-11-25 19:51:20| CRI

Kituo cha ushirikiano katika utunzaji wa mazingira kati ya China na Afrika kilizinduliwa jana hapa Beijing, na kuhudhuriwa na msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Deng Li na wajumbe wengine wa nchi za Afrika.

Bw. Deng Li amesema, kuzinduliwa kwa kituo hicho ni maendeleo mengine muhimu ya utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na kituo hicho kitakuwa jukwaa la pande mbili la kuimarisha mawasiliano ya sera za mazingira, kuhimiza ushirikiano na mawasiliano katika sekta ya uhifadhi wa mazingira na teknolojia husika, na kufanya utafiti wa pamoja kuhusu masuala ya mazingira.

Anatumai kuwa, kituo hicho kitainua kiwango cha mawasiliano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili, na kutilia nguvu mpya katika ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika.