China yachangia vifaa tiba kwa Sierra Leone ili kupambana na COVID-19
2020-11-25 18:30:15| cri

Ubalozi wa China nchini Sierra Leone jana Jumanne ulikabidhi mchango wa vifaa tiba kwa serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kupamabana na COVID-19.

Mchango huo ni pamoja na vitendanishi, vifaa vya kupumulia, barakoa, vifaa vya kujilinda na vinginevyo. Balozi wa China nchini Sierra Leone Hu Zhangliang amesema msaada huo ni moja ya hatua madhubiti za utekelezaji wa ahadi sahihi zilizotolewa na China kwenye Mkutano wa Kilele wa China na Afrika wa kupambana na COVID-19.

Waziri wa ulinzi wa Sierra Leone na Mratibu wa Taifa wa Mwitikio wa COVID-19 Kellie Conteh amesema nchi yake inafurahia kushirikiana na China katika kuboresha afya ya umma, na ana uhakika kwamba vifaa hivyo vitaimarisha huduma za afya kwa watu wa Sierra Leone