Kiwanda cha madawa cha China chazindua dawa za mitishamba nchini Kenya
2020-11-25 08:38:02| CRI

Kampuni ya madawa ya China, Jiangyin Tianjiang Pharmaceuticals, imezindua dawa ya mitishamba itakayotumika kuongeza kinga ya mwili, kutibu na kudhibiti homa ya mapafu.

Kampuni hiyo ambayo itafanya shughuli zake chini ya wakala wa Kenya, XRP Medical Kenya Limited, imetambulisha mchanganyiko wa dawa za asili za Healthouself Formula 3 na Healthouself Formula 5 nchini Kenya.

Meneja mkuu wa Kampuni ya XPR Medical Kenya Edgar Ngugi amesema, dawa hiyo itatumika kukinga na kuimarisha kinga ya mwili na kutibu aina zote za maambukizi kwenye mfumo wa hewa. Ameongeza kuwa, Bodi ya Madawa na Sumu (PPB) nchini Kenya imeidhinisha na kutoa kibali kwa bidhaa hizo mbili kuanza kuuzwa nchini humo.