China kujenga kituo cha msingi cha utafiti wa Mwezi katika kipindi cha nne cha mradi wa uchunguzi wa Mwezi
2020-11-26 18:29:48| CRI

Msanifu mkuu wa mradi wa uchunguzi wa Mwezi wa China, Bw. Wu Weiren jana alisema, China itajenga kituo cha msingi cha utafiti wa Mwezi katika kipindi cha nne cha mradi huo, ambacho kitaundwa na vyombo kadhaa vya uchunguzi vilivyoko katika obiti ya kuzunguka Mwezi na kwenye ardhi ya Mwezi.

Katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Safari za Anga na Anga za Juu la Kimataifa la Wenchang uliofungwa jana, Bw. Wu Weiren alisema, kituo hicho cha msingi kitakuwa na uwezo wa kufanya utafiti wa kisayansi kuhusu Mwezi na kuthibitisha teknolojia za kutumia rasilimali za Mwezi,  na vilevile kitafanya ushirikiano wa kimataifa katika kujenga kituo cha kimataifa cha utafiti wa kisayansi kwenye Mwezi.