UN: Kila sekunde 100 kijana mmoja mwingine ameambukizwa virusi vya HIV
2020-11-26 17:37:04| cri

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF imesema, mwaka jana, kila sekunde 100, kulikuwa na kijana mmoja mwenye umri wa chini ya miaka 20 aliyeambukizwa virusi vya HIV.

Ripoti hiyo imesema, mwaka jana, watoto na vijana karibu laki 3.2 waliambukizwa virusi vya HIV, huku laki 1.1 wakifariki kwa virusi hivyo.

Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Bibi Henrietta Fore amesema, idadi ya watoto na vijana walioambukizwa virusi vya HIV inaongezeka kwa kasi kubwa, na wengi kati yao wamefariki kutokana na ugonjwa huo. Kutokea kwa janga la COVID-19 kumesimamisha kazi za kukinga na kutibu UKIMWI na kuhatarisha uhai wa watu wengi zaidi.