Wafanyabiashara wa mbegu Uganda waitaka serikali kuunda sheria itakayooanisha sekta ya mbegu
2020-11-26 16:03:02| cri

Wafanyabiashara wa mbegu,kupitia Chama cha Wafanyabiashara wa Mbegu Uganda wameitaka serikali ya nchi hiyo kutoa hati za mbegu ili kuboresha harakati za kuvuka mpaka.

Kulingana na wafanyabiashara,hati hizo,sio tu zitatoa nafasi nzuri ya kukamilisha,lakini pia zitawezesha utekelezwaji wa itifaki za mbegu za Comesa na Afrika Mashariki.

Itifaki hizo zinalenga kuaonisha usafirishaji wa mbegu kati ya nchi za Comesa na Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa mwenendo wa mbegu katika eneo la Kawanda,wilaya ya Wakiso,Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara wa Mbegu Uganda,Bw Nelson Maseruka,alisema serikali inafaa kuunda sheria ambayo itaoanisha sekta ya mbegu ili kurahisisha biashara za mpakani.

Hata hivyo ,Kamishna ukaguzi mimea na uthibitishaji katika Wizara ya Kilimo , Bw Paul Mwambu, alisema japokuwa serikali imejitolea kuboresha sekta hiyo,mchakato wa uthibitishaji na utoaji hati unahusisha taratibu nyingi ,ambazo zitachukua muda kuzikamilisha.